WANAHABARI MWANZA WAKUMBUSHWA NAFASI YAO KATIKA KUPAMBANA NA RUSHWA
Na Tonny Alphonce,Mwanza
Kulekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) mkoa wa Mwanza imeanza kutoa elimu kwa makundi maalumu kwa lengo la
kuhakikisha jamii inapinga vitendo vyote vya rushwa na kuripoti dalili zote zinazo onyesha
viashiria vya rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya siku moja kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kupambana na rushwa, Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza James Ruge amesema vyombo vya habari vinajukumu kubwa la kuielimisha jamii juu ya rushwa na madhara yake katika ustawi wa taifa.
"Kwa hiyo ndugu zangu wanahabari tumeaita leo kisheria
kabisa kwa sababu sheria ya kupambana na
rushwa inaitaka TAKUKURU kushirikiana na wadau katika kutokomeza vitendo vya
rushwa na ndio maana kwa umuhimu wenu tumeamua kuwaita leo tuone namna gani
tutashirikiana ili kutokomeza vitendo vya rushwa.alisema Ruge"
Kwa upande wake mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Misungwi Elly Makala
amesema katika kipindi hiki cha uchaguzi wananchi wanapaswa kujua kuwa rushwa
ni kosa la jinai,ni kosa la kimaadili na pia rushwa ni kosa la kiimani hivyo
katika mazingira yoyote wasikubali kupokea rushwa kutoka kwa wagombea.
Elly amesema Uchaguzi wa serikali za mitaa ni uchaguzi muhimu kwa kuwa viongozi wanaoenda kuchaguliwa ndio chimbuko la iutawala bora na miradi mingi inafanyika katika ngazi hiyo ya mitaa hivyo viongozi ni vema wakawa waadilifu na waliochaguliwa kihalali.
Amesema serikali za mitaa zimeanzinzwa kwa lengo la kupeleka maendeleo
moja kwa moja kwa wananchi kama ibara ya 146 ya katiba ya jamuhuri ya muungano
wa Tanzania inavyosema.
Nae Edwin Soko mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mwanza Amewataka waandishi wa habari wasikubali kutumika katika kipindi hiki cha uchaguzi na badala yake wasimamie haki kwa wagombea wote watakaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali.
Kauli mbiu ya TAKUKURU ambayo ilitolewa na mheshiwa rais
inasema “Kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu,tutimize wajibu wetu” ikimtaka
kila mtanzania kuwa mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vya rushwa.
No comments