Breaking News

MBIO ZA MARATHONI YA MABADILIKO YA TABIANCHI 2024 KUTIMUA VUMBI SEPTEMBA 28 PANGANI,TANGA

 Na Tonny Alphonce,Mwanza

Zaidi ya kaya elfu hamsini  za jamii ya Pangani na Wamasai zilizoko mkoani Tanga zinatarajiwa kupewa teknolojia za kupikia kwa lengo la kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na kuhifadhi rasilimali za asili.

Hayo yamesemwa mkoani Mwanza na Sophia Donald mjumbe wa Muungano wa Jinsia  na Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania katika kikao na waandishi wa habari,amesema mpango huo umekuja baada ya kubaini kuna uharibifu mkubwa wa mazingira wilayani Pangani unaotokana na matumizi makubwa ya mkaa na kuni.

“Katika mpango wetu huu tumepanga kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa,kupunguza matumizi ya nishati mbaya za kupikia na kuboresha afya ya kina mama ambao ndio watumiaji wakubwa wa nishati mbaya za kupikia”.alisema Sophia

Sophia amesema ili kupata fedha za kuhamasisha jamii kutumia teknolojia safi ya kupikia, Muungano wa Jinsia  na Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania umeandaa mbio za Marathoni ya Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania 2024

Sophia Donald mjumbe wa Muungano wa Jinsia  na Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania akizungumza na wanahabari hawapo pichani.

“Tunategemea kuwa na wanariadha wa ndani na nje ya nchi na tutakuwa na mbio ndefu za kilometa 21,kilometa 10,kilometa 5 na kilometa 2.5 kwaajili ya watoto na watu wengine ambao sio wazoefu”.alisema Sophia

Nae Yohana Olinda Mwanachama wa Muungano wa Jinsia  na Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania ametoa wito kwa Watanzania kushiriki mbio hizo ili kuleta mabadiliko katika suala zima la mazingira.

Yohana Olinda Mwanachama wa Muungano wa Jinsia  na Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania kitoa wito kwa watanzania kujitokeza katika mbio za Marathoni ya Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania 2024

Mbali na kukimbia tutakuwa na mambo mengi siku hiyo ikiwemo maonyesho ya utamaduni wa Pwani na ule wa Wamasai kwa hiyo washiriki watapata nafasi ya kula vyakula vya asili.alisema Olinda

Amewtaka watanzania ambao watavutiwa na mbio hizo wapige simu namba 0745950950 kwaajili ya kujiandikisha na pia kupata maelezo ya ziada kuhusiana na mbio hizi za Mbio za Marathoni ya Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania 2024.

Mbio za Marathoni ya Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania 2024 zinafanyika kwa mwaka wa pili mfululizo ambapo mwaka jana mbio hizi zilifanyika mkoani Iringa na Mwaka huu zinafanyika mkoani Tanga zikiwa na lengo la kuihamasisha jamii kutunza mazingira.

 

No comments