Breaking News

WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI TPDC WATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO INAYOFADHILIWA NA TPDC - MTWARA

 


Muonekano wa moja ya jengo la Kituo cha Afya Msimbati ambalo linaendelea kujengwa.

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za kijamii kwenye maeneo ambayo shughuli za utafutaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa gesi aislia zinafanyika. Huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo afya, elimu, maji na utawala bora zinaimarishwa ikiwa ni sehemu ya Uwajibikaji wa Shirika kwa Jamii (CSR). 

Hayo yamebainishwa Juni 12,2024 Katika ziara ya wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya TPDC walipotembelea  miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na TPDC kwa kupitia mpango wa uwajibikaji wa Shirika kwa Jamii yaani  ‘‘Corporate Social Responsibility’’ Mkoani Mtwara.

Akitoa ufafanuzi wa miradi hiyo Meneja mradi Muhandisi Omari Kitiku  alieleza kuwa "TPDC ilisaini hati ya makubaliano (MoU) ya utekelezaji wa miradi yenye thamani ya Tsh 1,284,376,130  ambayo inatekelezwa katika kata ya Msimbati na Madimba , Makubaliano hayo yalihusisha Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara  kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha kata ya Msimbati, Jeshi la Polisi Tanzania kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Msimbati pamoja na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa ajili ya uwekaji wa taa za barabarani katika vijiji vya Msimbati, Mngoji na Madimba’’.

Aidha, Mhandisi Kitiku aliongeza kuwa "gharama za ujenzi wa miradi hiyo zinatofautina kulingana na aina ya mradi kama ‘Ujenzi wa kituo cha Afya unagharimu Tsh 600,000,000/= ambapo umefikia asilimia 80% ya ujenzi,  Ujenzi wa kituo cha Polisi unagharimu  Tsh 186,170,803 na umefikia asilimia 65%  pamoja na uwekaji wa taa za barabarani Tsh 498,205, 327 umefikia asilimia 15%. 
Mhandisi Omari Kitiku akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya kwa wajumbe ya Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa TPDC Bwn Ally Mluge alieleza namna TPDC inavyoshirikiana na jamii ikiwa ni pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kuleta ustawi wa jamii na kuboresha mahusiano mazuri yaliyoyopo kati ya TPDC na jamii zinazopitiwa na miundombinu ya gesi asilia. 

"Utekelezaji wa miradi hii ni sehemu ya Jitihada za TPDC katika kukuza na kuboresha huduma na  mahusiano na jamii zinazopitiwa na miundoimbinu ya gesi asilia’",aliongea Mluge.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi ya TPDC, Viongozi wa Halmashauri, wakandarasi na timu ya mradi ya TPDC. 

Katika hatua nyingine Mhe. Rashidi Omary Linkoni, Diwani wa Kata ya Msimbati alishukuru uongozi wa TPDC kwa kuendelea na jitihada za kuimarisha huduma za kijamii katika maeneo ambayo yanapitiwa na miundombinu ya gesi asilia. “TPDC kupitia jitihada zake za kusaidia jamii, inaongeza chachu ya kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma hizo katika maeneo yetu, kwa hatua hii, naipongeza TPDC na tunaomba iendelee na jitihada hizi”. alisema Mhe. Linkoni.
Muonekano wa jengo la Kituo cha Polisi cha Msimbati  linaloendelea kujengwa kwa ufadhili wa TPDC

No comments