MADIWANI WAFURAHISHWA NA UZINDUZI WA PROGRAM YA MALEZI NA MAKUZI HALMASHAURI YA MADABA WATAKA JAMII IPOKEE
Joyce Joliga,Songea
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Teofanes MlelwaT amezindua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto( PJT-MMMAM) ngazi ya Halmashauri katika Ukumbi wa halmashauri hiyo na kuwataka wananchi kuwekeza katika malezi na makuzi ya awali ya mtoto katika halmashauri hiyo hivyo kupunguza udumavu.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Madiwani,Wakuu wa idara,Watumishi wa Halmashauri amoja na waandishi wa habari na viongozi mbali mbali wa dini, vyama vya siasa na wananchi,alisema Madiwani wa halmashauri hiyo wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa program hiyo kwani inafaida kubwa kwa jamii na waifanye kuwa ni yao ili kuweza kujenga jamii yenye ustawi bora.
Mwenyekiti huyo ameshukuru kwa (PJT-MMMAM) kuzinduliwa ndani ya Halmashauri na ameitaka kamati ya Mkoa inayotekeleza program hiyo kuhakikisha inatoa elimu hiyo kwa Madiwani , watumishina kwenda hadi ngazi ya jamii ili kusaidia jamii iweze kupata elimu juu ya malezi ya watoto ambao umri wao ni kuanzia mwaka 0-8 kwa mujibu wa program hii. Ili tukawe mabalozi kwa wananchi wengine kwa kuwapa elimu juu ya utekelezaji wa (MMMAM) katika jamii zetu.
Awali akitoa mada wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani jana kwa niaba ya ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa, Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Mariam Juma amesema kuwa watoto ili wakue vizuri kimwili,kiakili,kihisia, kimaadili, afya na lishe lazima yawe sawa hivyo wazazi ni wajibu kulisimamia hilo kwa namna moja au nyingine katika jamii ili tupate kizazi chenye afya njema na maadili kwa miaka ijayo.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Mariam Juma akitoa mada wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani
Ameongeza kuwa ulinzi na usalama wa mtoto ni jukumu la kila mzazi na jamii nzima inayomzunguka mtoto ambapo amewataka wananchi kubadirika na kuacha kuficha vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa Watoto kwa kuripoti matukio hayo kwenye vyombo vya dola ili kutokomeza au kupunguza vitendo hivyo.
Naye Diwani kata ya Mkongotema Vastus Mfikwa,amepongeza serikali kupitia wizala ya maendeleo ya jamii kwa kuanzisha program ya malezi na makuzi ya Mtoto ambapo amesema wameipokea kw mikono miwili na ameomba wapatiwe semina nyingine ili waweze kupata elimu zaidi ambayoitawasaidia kwenda kutoa kwenye kata zao.
Naye Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mussa Rashid ,alisema kuzinduliwa kwa program hiyo kutasaidia kuongeza ufanisi kwa wataalam wa afya kutoa huduma bora zaidi kwa wajawazito na watoto wa umri chini ya miaka mitano kwani watoto wataweza kupelekwa kliniki kwa wingi, ufatiliaji utaongezeka ngazi ya jamii ,hivyo watoto kupata chanjo zote zinazotolewa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitalini na pia itasidia kupunguza udumavu kwa watoto wenye umri wa miaka 0-8.
Hatua hii ya uzinduzi wa MMMAM katika ngazi ya halmashauri ni Utekelezaji wa Programu ya Taifa ya MMMAM ambapo uzinduzi ulianzia ukashuka ngazi ya ngazi ya Taifa,Mkoa na kwa sasa uzinduzi umeshuka katika ngazi ya Halmashauri.
No comments