WAZAZI WATAKIWA KUHAKIKISHA WATOTO WANAPATIWA CHANJO ZOTE MUHIMU
Na Tonny Alphonce, Mwanza
Inaelezwa
kuwa utoaji Chanjo kwa watoto kila mwaka huokoa maisha ya watoto wafikiao milioni
3 kila mwaka.
Mtoto akipatiwa
Chanjo humkinga maradhi mbalimbali ukiwemo ulemavu na vifo vitokanavyo na
magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ikiwa ni pamoja na surua, homa ya ini
(hepatitisi B), dondakoo, kifaduro, nimonia, polio, kuhara kunakosababishwa na
virusi vya rota, rubela na pepopunda.
Kisayansi
chanjo ni kitendo cha kupewa kinga mwili kwa njia ya kuamsha vitoa kinga viwe
tayari kupambana na adui ambaye wanamjua tayari.
Kwa kuliona
hilo Shirika la DUNIA RAFIKI lenye makao yake makuu yake mtaa wa veta,
Buhongwa, wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Zahanati ya Shadi
pamoja na wahudumu wa afya liliendesha zoezi la utoaji wa matone ya Vitamin A
kwa watoto wenye umri wa miezi 8 hadi miaka 4katika kituo cha malezi MTOTO WETU
ambapo watoto 43 walipatiwa matone hayo.
Akizungumzia
zoezi hilo mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Sophia Hamisi Asenga amesema mara
baada ya kufuangua kituo cha Kijamii cha malezi, MTOTO WETU katika eneo hilo la
Luchele na kuanza kupokea watoto na kuwapa huduma za ujifunzaji wa awali,
lishe, afya, uchangamshi, malezi pamoja na ulinzi na salama kwa watoto wenye
umri wa miaka 3-4 waligundua baadhi ya watoto kuwa na matatizo ya kiafya na
ukuaji.
Tulipoanza kuwapokea
watoto hawa wenye umri wa miaka 3-4 tulianza kuona changamoto mbalimbali
zinazowakabili watoto wanaofika kituoni,wengine walikuwa na changamoto za
kiafya na wengine walikuwa na changamoto ya ukuaji na ndipo nikaona ni vema
niwalete wataalamu wa afya waweze kuwapima watoto na kuzungumza na wazazi na
walezi ili tuweze kuwasaidia watoto ambapo tulibaini kuna watoto hawajapatiwa
chanjo yoyote katika ukuaji wao.alisema Sophia
Kabla ya kuanza Zoezi la kuwapatia chanjo watoto wataalamu wa afya walitoa elimu kwa wazazi na walezi wa watoto zaidi ya 41 juu ya umuhimu wa matone ya Vitamin A kwa watoto wenye umri chini ya miaka 4 ambapo wazazi, walezi na wajawazito walipata elimu hiyo na baadaya elimu hiyo kwa pamoja walikubaliana watoto wao wapatiwe chanjo hiyo yam atone
Akizungumza kabla
ya utoaji wa chanjo hiyo mhudumu wa afya wa mtaa wa Nganza. Bi. Consolata Ligola
alisema upungufu wa Vitamin A mwilini husababisha madhara mengi kwa mtoto
ikiwemo ukosefu wa kinga mwilini, hivyo mtoto kuwa katika hatari ya kupata magonjwa
mara kwa mara, kutoona vizuri katika mwanga hafifu.
Bi. Consolata
aliendelea kusema, bado elimu inatakiwa kwa jamii ili kuhamasisha wananchi
kutumia vyakula vyenye vitamini A kwa watoto, ili kuepukana na matatizo ya
lishe duni yanayowakumba watoto wengi wanaoishi pembezoni.
Nae
mwenyekiti wa Mtaa wa Nganza, ndugu Phinias Mayingu alisema wao kama viongozi
wa serikali ngazi ya chini ni wajibu wao kuhakikisha wananchi wanapata huduma
bora na kwa wakati.
Nimefurahishwa
na zoezi hili la kutoa majone ya Vitamin A kwa watoto hapa kituoni, nawapongeza
sana walio ratibu zoezi hili, nina toa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi pale
inapotokea fursa kama hizi zinazo walenga watoto kwani ni haki yao ya msingi
kupata kupata huduma zote muhimu za afya katika ukuaji wao”alisema Mayigu
Kutokana na
umbali wa kufika katika zahanati
ya Shadi ambapo wazazi hulazimika kutembea umbali wa kilometa 2-3 na wengi
kushindwa kufika wamefurahia kusogezewa huduma hiyo ya utoaji matone kwa watoto
wao.
“Tuna
shukuru sana kwa huduma hii na tunatamani iwafikie watoto wengi zaidi, kuna
watoto wengi wapo mtaani hawapati huduma hii kutokana na changamoto mbalimbali
za maisha, ukosefu wa elimu juu ya umuhimu wa matone ya Vitamin A na madini
lishe mengine elimu niliyo ipata leo sitabaki nayo peke yangu bali
nitawaelimisha wengine na kuhamasisha pia”. Alisema Ester
Ester amesema
anakiri kuwa kumekuwa na maneno mengi ya upotoshaji kuwa chanjo ama matone
yanamadhara kwa watoto ikiwa ni pamoja na kuua kizazi lakini baada ya kupata
elimu hiyo amegundua kuwa maneno hayo hayana ukweli wowote.
Mwaka 2022
mkoa wa Mwanza ulitoa chanjo kwa watoto 965229 ili kuwakinga na ugonjwa Polio
ambapo mkoa uliweza kuvuka lengo kwa asilimia 114 na hii ilitokana na jamii
kupata elimu ya kutosha.
Kutatuliwa
kwa changamoto za kiafya kwa watoto ikiwemo kupatiwa chanjo zote muhimu kutaenda
sambamba na malengo ya mpango wa Taifa wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali
ya Mtoto ambao unajikita katika kutatua changamoto za ukuaji wa mtoto katika
ukamilifu wake kuanzia mwaka 0-8
No comments