Breaking News

HALMASHAURI 7 ZA TANGA ZA ZAKAMILISHA UZINDUZI WA MMMAM

                                                                Raisa Said,Tanga

Jumla ya Halmashauri saba kati ya halmashauri 11 zilizoko mkoani Tanga zimekwisha zindua Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Mendeleo ya Awali ya Mtoto tangu program hiyo ilipozinduliwa  mkoani Tanga Oktoba, mwaka jana.


Akzingumza katika mahojiano jijini Tanga, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa, Mmasa Malugu azitija Halmashauri hizo kuwa ni pamoja na Tanga Jiji, Mkinga, Pangani na Korogwe Mjini..

Malugu, ambaye ndiye Mratibu wa Program hiyo mkoani Tanga kwa kushirikiana na Asasi ya United Help for Tanzania Children (UHTC) alizitaja Halmashauri nyingine kuwa ni Korogwe Vijijini, Lushoto na Bumbuli.

Alisema kuwa halmashauri nyingine ambazo ni Muheza, Kilindi, Handeni Mjini na Handeni Vijijini zitazindua program hiyo katika awamu ya pili ya mpango huo.

Akizungumzia juu ya umuhimu wa program hiyo, alisema miongozo ambayo imetolewa na serikali inalenga kuwekeza  katika maeneo ya kuboresha ulinzi na usalama, ujifunzaji wa awali, lishe, afya na malezi yenye cyenye mwitikio ambayo yanaweza kumjengea mtoto kujiamini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo wilayani Mkinga, Ofisa Elimu, Awali na Msingi ilaya ya Mkinga, Omari Mashaka alisema program hiyo imekuja wakati muafaka na utawasaidia walimu kutekeleza majikumu kwa ufanisi..

“Tu na changamoto kubwa sana. Sasa hivi kuna watoto hawafundishiki. Mtoto anarudia darasa mara mbili, mara tatu mpaka inafikia hatua tunatumia maafisa walisomea elimu maalum ili kujua mtoto anachangamoto gani ambayo inamuathiri asiweze kufundshika,” alisema.

Alisema mtoto anapojifunza anatumia milango mitano ya fahamu na milango yote inapokuwa inafanya kazi hata ufundishwaji unakuwa rahisi.

Alisema umri wa miaka sifuri hadi nane, hasa darasa la awali hadi la pili, ni eneo muhimu ambalo wanasisitizia ufundishaji wa watoto hawa hasa katika mahiri za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini, Sadiki Kalage akitangaza kuipokea program hiyo, alisisitiza juu ya umhimu wa kushirikisha madiwani na watendaji katika ngazi kata na vijiji pamoja na wenyeviti wao katika utekelezaji wa program hiyo ili elimu hiyo ifike chini.

“Zoezi hili pamoja na kuwa ni la muda mrefu litasaidia utaratibu wa kukuza watoto. Litaweka utaratibu watoto wanakuanie au wana shida, kwa nini watoto wkizaliwa wasikue hadi wawe wakubwa kama sisi,” alisema.

Alisititiza idara husika katika program hiyo kutenga bajeto kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za program hiyo.  

Naye  Mkurugenzi wa UHTC, Dk Regis Temba alisema watoto mkoani Tanga wako katika ukuaji timilifu ni asilimia 44 na akasisitiza kuwa wao kwa kushirikiana na serikali wamejipanga kutoa elimu mbalimbai ya malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto ili watoto wa mkoa wa Tanga  wapate malezina makuzi timilifu.

No comments