WAZAZI SHIRIKIANENI NA WALIMU WA AWALI KUTENGENEZA ZANA ZA KUJIFUNZIA WATOTO WA AWALI
Na Joyce Joliga,Songea
Wazazi kata ya Ruhuwiko Manispaa ya Songea wameshauriwa kusaidiana na walimu wa madarasa ya awali kutengeneza Zana za kujifunzia watoto wao ili kuwasaidia kuweza kujua kusoma,kuandika na kuhesabu kwa njia nyepesi zaidi,kwani vifaa hivyo havigharimu pesa yoyote vipo kwenye maeneo yao.
Wito huo umetolewa na Diwani kata ya Ruhuwiko Wilbard Mahundi wakati wa akizungumza na mwandishi wa habari hii ambapo aliwataka kamati ya maendeleo ya elimu ya kata kuhakikisha inashirikiana na Wazazi kujitolea kutengeneza vifaa mbali mbali vya kujifunzia watoto kuhesabu kwa kutumia visoda,mabunzi, vijiti Vizio vya soda ,kuchora michiro mbalimbali ya wanyama,mimea, nyumba na hata matunda.
Alisema,Wazazi wakishiriki kutengeneza dhana za kujifunzi kutaleta hamasa kubwa kwa walimu na watoto wao hivyo siyo dhambi kama watashiriki kwenye zoezi hilo.
"Niwasihi sana wazazi wenzangu ambao tuna muda tujitokeze kusaidiana na walimu kutengeneza vifaa mbali mbali vya kujifunzia watoto wetu ili waweze kusoma kwa vitendo na kuelewa haraka,"Alisema Mh.Mahundi
Naye Anna Anosisye mkazi wa Ruhuwiko alisema Kuna kila sababu wazazi kujitolea kutengeneza Zana hizo kwani zinawasaidia watoto kupenda kwenda shule kujifunza kwa vitendo na wanaelewa zaidi tofauti na kusoma tu.
"Watoto wanavutiwa na mandhari nzuri za michiro na uwepo wa Zana mbalimbali kwenye darasa unawasaidia kuwa making zaidi na masomo hivyo kupenda kujifunza zaidi."Alisema Anosisye
Naye Victor Maganga amewashauri wazazi kupenda kufatilia na kuwekeza kwenye elimu za watoto wao wa awali kwani ndio msingi imara wa maendeleo ya mtoto na kuacha kuwaachia kila kitu walimu peke
Mtaala wa Elimu ya Awali umezingatia kwamba elimu bora ya awali ni muhimu
kwa maisha ya mtoto.
Mtoto akijenga msingi imara wa kujifunza katika Elimu ya
Awali atakuwa tayari kuanza darasa la I na kuendelea vizuri katika ngazi zingine
za elimu
No comments