WANANCHI WALIA KITUO CHA AFYA HAKITOI HUDUMA LICHA YA UJENZI WAKE KUKAMILIKA
Na Tonny Alphonce, Sengerema
Wananchi wa
kijiji cha Kanyerere wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wamekuwa wakilazimika
kutembea umbali wa kilometa 15 kufuata huduma za mama na mtoto kutokana na kituo
cha afya cha Kanyerere kutofanyakazi licha ya ujenzi wake kukamilika.
“Kama unavyoona
kila kitu wananchi tumechangia lakini hakuna daktari yoyote aliyeletwa hapa
hakuna dalili ya dawa kuletwa hapa na kina mama wajawazito na watoto ndio
wanaoteseka katika upatikanaji wa huduma za afya”.alisema Marrytilida
Marrytilida amesema
kutokana na umbali wa kupata huduma za mama mjamzito katika kijiji hicho
wananchi wamekuwa wakilazimika kwenda kupata huduma Busilasoga au Igaka na
kusababisha baadhi ya kina mama kujifungua wakiwa njiani na kuhatarisha maisha
ya mama na mtoto.
Kwa upande
wake Nassari Mkoloka mkazi wa kijiji hicho cha Kanyerere amesema wanachohitaji
hivi sasa ni wataalamu wa afya ambao watatoa huduma katika kituo hicho.
“Haiwezekani tukaendelea kuishi hapa bila
kupata huduma wakati michango ya kufanikisha ujenzi tulitoa sasa tunashangaa jengo
limekamilika lakini bado hakuna dalili zozote za kuanza kutupa huduma hapa”.alisema
Mkoloka
Akitolea ufafanuzi
wa kuchelewa kuanza kutoa huduma kwa kituo hicho cha afya Kanyerere mkurugenzi wa
halmashauri ya Sengerema Binuru Shekidele kuchelewa kuanza kazi kwa kituo hicho
kumesababishwa na baadhi ya vijiji kushindwa kuchangia fedha za kukamilisha
ujenzi wa kituo hicho cha afya.
“Mhe waziri kwa mujibu wa mujibu wa taratibu za TASAF
,mradi huu wananchi walitakiwa kuchangia asilimia 10 na TASAF asilimia 90
,sasa kuna baadhi ya vijiji vinasuasua
kuweka nguvu zao ndio maana mradi huu unachelewa kuanza kwa wakati”. Alisema Binuru
Nae mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Sengerema Marco Makoye amesema kitendo cha jengo kukamilika na
kutokutoa huduma ni kitendo cha watendaji kuichonganisha serikali na wananchi.
“Hapa watu
wanaona majengo tena yamekamilika na watu wanatembea kilometa 15 kwenda kupata
huduma hivi CCM tukirudi kuomba kura tutapewa kweli”.alisema Makoye
Akizungumza
na wanachi hao wa kijiji cha Kanyerere Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mohammed Mchengerwa amesema haoni sababu ya
msingi ya kucheleweshewa wananchi huduma wakati kituo kimekamilika kwa asilimia
96.
“Kwa hiyo maelekezo
yangu mkurugenzi jiongeze na ujiamini nikirudi tena na kukuta jambo hili
halijafanyiwa kazi nitakusimamisha umepewa nafasi hii na Mh Rais msaidie
wananchi wasikose huduma kwa uzembe wa watu wachache”.alisema Mchenjerwa
Kutokana na
kutoridhika na maelezo ya mkurugenzi Mchenjerwa amesema kinachoonekana katika
mradi huo ni waliopewa dhamana kushindwa kusimamia zoezi la ujenzi wa kituo
hicho na akatoa siku 14 kuhakikisha kituo hicho kinaanza kutoa huduma za awali
kwa wananchi.
“Katibu tawala
nakuagiza simamia zoezhili waandikie barua wahusika wote ili mradi huu uanze,h atuna
sababu ya kuwapa hasira wananchi wetu kituo wanakiona lakini wanaendelea
kuteseka kupata huduma za afya”.alisema Mchenjerwa
Pamoja na changamoto ya kijiji cha Kanyerere huduma za afya ya mama na mtoto zimeendelea kuimarika wilayani Sengerema huku kiwango cha wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya afya ikiongezeka ambapo kati ya wanawake wajawazito wanane hadi kumi hujifungulia hospitali kila siku.
vifo vya kinamama wajawazito navyo vimepungua kutoka 11/100000 mwaka 2014,8/100000 disemba 2015,6/100000 hadi kufikia juni 2017 vifo vimeripotiwa 3/100000.
Kutatuliwa kwa
changamoto hiyo ya kituo cha afya katika kijiji cha Kanyerere wilayani
Sengerema mkoani Mwanza kutaenda sambamba na malengo ya mpango wa Taifa wa
Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ambao unajikita katika kutatua
changamoto za ukuaji wa mtoto katika ukamilifu wake kuanzia mwaka 0-8
No comments