Breaking News

MATINYI: SERIKALI INALIFANYIA KAZI SUALA LA UCHUMI WA WANAHABARI

 Na Tonny Alphonce,Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Melezo Mobhare Matinyi  amewataka waandishi wa habari na wamilikiwa vyombo vya habari nchini  kubadili mfumo wa uendeshaji wa kazi  zao ikiwa njia moja wapo ya kuwakomboa kiuchumi kama zilivyo taasisi nyingine.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Melezo Mobhare Matinyi akizungumza na washiriki wa mkutano mkuu wa wanachama wa muungano wa klabu za waanshi wa habari Tanzania (hawapo pichani)

Matinyi amesema Serikali upande wake inafahamu kuhusiana na hali mbaya ya kiuchumi waliyonayo waandishi wa habari na ndio maana kupitia kamati iliyoundwa na waziri wa mawasiliano  na sayansi ya habari itakuja na majibu ya nini kifanyike ili kubadili hali hiyo.

"Tayari tume hiyo iimeishakamilisha kazi yake na ipo kwenye hatua za mwisho na ifikapo mwezi januari 2024 itatujulisha".alisema Matinyi

Matinyi amesema ili nchi iweze kuendelea inatakiwa kuwa na vyombo vya habari imara  hivyo serikali imedhamilia kuja na majibu ya changamoto hiyo

Matinyi amewataka waandishi wa kuandika habari za maendeleo ili kusindikiza maendeleo ya nchi na tayari maafisa habari wa serikali wametakiwa kuanza kujipanga na aina hizo za habari zinazochochea maendeleo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, rais ya Klabu za waandishi wa habari Tanzania Deogratius Nsokolo, ameiomba Serikali kuendelea kujenga mazingira wezeshi kwa vyombo vya habari ili viendelee kutekeleza wajibu wao kikatiba wa kutoa habari na kutafuta habari.



Rais ya Klabu za waandishi wa habari Tanzania Deogratius Nsokolo akikmkaribisha mgeni rasimi na kutoa neno la utangulizi.

Nsokolo amesema kuwa waandishi wa habari nchini ni muhimili muhimu na wanayo haki ya kutoa habari na kupata habari hivyo serikali inawajibu wa kuwalinda wanahabari na kuhakikisha kuwa wapo salama wakati wote.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Keneth Simbaya, amewakaribisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kuunganisha nguvu kwa pamoja na kuwatumikia wananchi kupitia sekta ya habari ambayo ni husafirisha taarifa kwa haraka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Keneth Simbaya akitoa neno la utangulizi katika mkutano mkuu wa wanachama wa muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania

“Tumejipanga kuendelea kufungua milango kwa wadau na kujibidisha ili kuendelea kuzikuza Klabu za waandishi wa habari Tanzania, hali itakayochangia kuwafikia wananchi na kupaza sauti zao kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini”alisema Simbaya

Picha ya pamoja ya waratibu wa Klabu za waaandishi wa habari Tanzania






Picha ya pamoja ya Waweka Hazina wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania

Picha ya pamoja ya makatibu wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania

No comments