KEMEENI MILA NA DESTURI ZINAZOKANDAMIZA WATOTO WA KIKE
Joyce Joliga,Songea
Jamii
imeshauriwa kukemea Mila na desturi potofu ambazo zimepitwa na wakati wanafanyiwa watoto wa kike ikiwemo kutopelekwa shule,kukeketwa na
kufundishwa mafunzo yasiyofaa katika umri mdogo wa miaka 5-8,kwani vitendo
hivyo ni vya ukatili na havifai kufumbiwa macho.
Wito huo umetolewa wakati wa siku ya Mtoto wa kike duniani na Mkurugenzi wa Faraja toto ,Alfrida Msemwa wakati akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema,jamii
inapaswa kuwaangalia watoto wa kike kwa jicho la tatu ili waweze kufanikiwa
kwenye elimu ,na maisha yao ya baadaye.
"Jamii
inapaswa kuwathamini na kuwasaidia watoto
wa kike ,kwa kuwalea katika maadili mema, na kuwasaidia kupata elimu ili
waweze kufanikiwa kutimiza ndoto zao ,"alisema Faraja
Aidha wazazi wametakiwa kuwajengea uwezo watoto wa kujiamini na kusoma kwa bidii ili kuweza kutimiza ndoto zao pindi watakapokua wakubwa.
Naye Anna
Gabriel mkazi wa Namtumbo amewashauri wazazi kutoa haki Sawa kwa
watoto wote bila upendeleo,na kuondokana
na fikra potofu kuwa kumsomesha mtoto wa kike
ni kupoteza muda kitu ambacho si sahihi.
Kwa upande wake mtaalam
wa malezi na makuzi ya mtoto Davis
Gisuka ametoa ushauri kwa wazazi na
walezi kuendelea kuwalea watoto kwa
pamoja ikiwa ni pamoja na kuwathamini kwani watoto wote nisawa.
Alisema,Katika
jamii nyingi za kitanzania watoto wa kike wamekuwa wakipewa kazi nyigi sana za
nyumbani kuliko wa kiume
Hali hii
husababisha mtoto wa kike kukosa muda wa kujisomea kulinganisha na mtoto wa
kiume..
Mwisho.
No comments