JINSI BAJETI KATIKA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA KITAIFA YA PJT-MMMAM ITAKAVYOONGEZA UWEKEZAJI WA MALEZI NA MAKUZI YA WATOTO (0-8)
NA HADIJA OMARY, DODOMA
Nchini Tanzania asilimia 45 ya watoto wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu za ukuaji kutokana na viashiria mbali mbali vya hatari vya maendeleo kama vile utapiamlo, umasikini, kukosa uhakika wa chakula , msongo wa mawazo ya kifamilia .
Miundombinu duni na uhaba wa rasilimali pamoja na kutelekezwa na unyanyasaji wa watoto, ili kushughulika na changamoto hizi , program ya malezi jumuishi inahitaji kupewa kipaumbele na kuratibiwa vyema
"Tafiti zinaonyesha kuwa kwa kila dola 1 ýa marekani inayowekezwa kwenye afua za programu jumuishi ya kitaifa ya PJT-MMMAM , inaweza kuzalisha hadi dola 17. Aidha ushaidi unaonyesha kwamba uwekezaji katika Elimu ya awali kwa watoto walio katika mazingira hatarishi unarudisha faida inayokadiliwa kuwa na asilimia 7 hadi 16 kwa mwaka.
Kufuati hali hii Serikali hapa Nchini Tanzania imeona umuhimu kuendelea kuwekeza katika maswala ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kupitia program jumuishi ya kitaifa ya PJT-MMMAM katika kutenga bajeti kuanzia ngazi za halmashauri
Program jumuishi ya kitaifa ya MMMAM inatoa mchango mkubwa katika kufanikisha mpango wa Taifa wa maendeleo ya miaka mitano (2021/22-2025/26) kwa kutambua kwamba watoto ambao wanakosa kufikia kikamilifu hatua za ukuwaji ni changamoto kwa maendeleo ya Taifa na tishio kwa malengo ya kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na jitihada za kujenga Nchi yenye hadhi ya uchumi wa kati.
Hata hivyo kutokana na chapisho la The Lancet imegundulika kuwa "asilimia ya watoto waliokwenye hatari ya kutofikia ukuwaji wao timilifu wapo kwenye hatari ya kushusha wastani wa kipato chao kwa asilimia 26 watakapofikia utu uzima swala ambalo litashusha hali ya uchumi na kuweka familia kwenye mtego wa kiumasikini.
Licha ya program hiyo kuzinduliwa miaka miwili iliyopita mwaka 2021 na kuendelea na utekelezaji wake na kupata mafanikio kadhaa yatokanayo na mpango huo lakini Bajeti ya utekelezaji wa mpango huo imekuwa ikifanywa na serikali kuu kupitia wadau wa kisekta ambazo ni Elimu, Afya , Lishe, ulinzi na usalama na malezi yenye maitikio kwa kushirikiana na wadau wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali children in cross fire (CIC), Tanzania Ecd Network (TECDEN) .
Hali hii inamsukuma Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Doroth Gwajima kupitia Mkutano wa kitaifa wa wadau wadau watekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto PJT-MMMAM uliofanyika Desemba 11/12/2023 Jijini Dodoma kuziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) inayolenga watoto kuanzia umri wa miaka 0 mpaka 8.
Dkt Dorith Gwajima amesema Halmashauri ziweke mikakati ya kuingiza afua za PJT-MMMAM katika bajeti ya Serikali ya 2024-2025 ambapo mchakato wa maandalizi ya bajeti umeshaanza kwenye ngazi za tawala za Mikoa na Serikali za mitaa.
Pia ameongeza kuwa, Mikoa ipange mpango na utaratibu wa kuzifikia Halmashauri zote 184 ambapo mpaka sasa zimeshafikiwa Halmashauri 70 baada ya kukamilikasha uzinduzi wa PJT-MMMAM katika ngazi za Mikoa.
Amesema programu hiyo ni muhimu kwa ukuaji timilifu wa mtoto na mkurugenzi atakayeshindwa kupata bajeti hiyo atakuwa anachangia sababu zinazoweza kusababisha mtoto asiweze kukua katika utimilifu wake
Pamoja na maelekezo ya utengaji wa bajeti kuanzia ngazi za halmashauri lakini anawataka wadau wanaohusika katika program hii kuhakikisha wanafanya kazi kama timu kwa kuratibiana vizuri, kwa kuwa malengo ya program ya MMMAM hayawezi kufikiwa bila kuzishirikisha sekta zote kwa uwiano na umuhimu unaofafana na kuwataka waliopewa dhamana ya uratibu kuunganisha timu ya utekelezaji ili kupata mafanikio makubwa zaidif.
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni Wadau muhimu katika utekelezaji wa programu hii, ambapo amewataka kuongezeni jitihada ya kuwekeza katika program hii kwa kushirikiana na Serikali katika ngazi zote. Aidha, Waandishi wa habari vinara kupitia umoja wenu endeleeni kuelimisha jamii kuhusu program hii ili jamii ielewe umuhimu wa malezi na makuzi yenye tija kwa watoto wetu.
Craig Ferla ni mkurugenzi mkazi kutoka shirika la Childrens in Crossfire amesema wakati program hiyo ikizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2021 hakukua na bajeti kabisa licha ya kuwepo na mafanikio kadhaa katika utekelezaji wa program hiyo kwa miaka hii miwili ya utekelezaji wake .
"Tukielekeza jicho la kipekee kwenye ajenda ya MMMAM tutapata matokeo makubwa kwani kinachonifurahisha zaidi ni kuona viongozi wote wapo kwenye mstari wa mbele kwenye maswala haya ambapo taarifa ya utekelezaji kwa miaka miwili ya program inatia matumaini licha ya kuwepo kwa changamoto hiyo ya bajeti lakini kazi kubwa iliyofanyika inaonekana .
Licha ya kuwepo na mafanikio kadhaa yaliyofikiwa na programu hii ya kitaifa ya PJT-MMMAM ikiwa pamoja na kufanya uzinduzi wa program kwa Mikoa yote 26 ya Tanzania bara pamoja na kujenga uelewa katika halmashauri 70 bado changamoto ya Bajeti imekuwa ni changamoto katika utekelezaji wa mpango huo kama anavyoeleza Nelson choaji Mratibu wa programu kutoka shirika lisilo la kiserikali la Lindi women paralegal (LIWOPAC) .
Anasema changamoto iliyopo kwa sasa katika kukabiliana na hali ya bajeti ni kwamba inashindwa kuwezesha wadau kufika katika maeneo ya chini zaidi hali inayopelekea hata wadau wa halmashauri kushindwa kupanua wigo katika kutekeleza afua za MMMAM
"Tumewahi kufanya mazungumzo ya kutosha na viongozi wenzetu wa Serikali na watumishi kuwaomba watumie bajeti zao za ndani ili kuweza kutekeleza mpango huo katika halmashauri zao lakini changamoto kubwa ilikuwa ni kwamba hawakuwa na Aprove yoyote ya kuhusu matumizi ya bajeti katika afua hizo,
"Walikuwa wakisema wanasubiri miongozo kutoka Serikali kuu ambayo itaaijisha vipaumbele vya bajeti ya utekelezaji leo tumepata mwanga baada ya wizara kuhaidi kufanya jitihada za makusudi za kuhakikisha kwamba kutaandaliwa miongozo ambao utaonyesha sekretarieti za mikoa zinapopokea bajeti kutoka halmashauri pia ziainishe afua za MMMAM "
Device Gusaka ni mtaalamu wa maswala ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kutoka shirika lisilo la kiserikali la TECDEN anaipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kutenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa program hii ya kitaifa ya PJT-MMMAM
Hata hivyo anasema ili kufikia malengo yanayokusudiwa ni vyema kwa hizo halmashauri zikaangalia sehemu ambayo inapwaya katika yale maeneo makuu yaliyopangwa kufanyika katika utekelezaji wa program hii ya kitaifa ya MMMAM
"Kabla ya kupanga bajeti ni vizuri wakazipitia vizuri zile kazi zilizopangwa kufanyika kupitia mpango huo wakazielewa vizuri wakaangalia wapi kuna gap kati ya hizo ni ipi wataipa kipaumbele.
Utekelezwaji wa bajeti ya Programu Jumuishi ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali Ya Mtoto katika halmashauri zote nchini utatoa uhakika wa mtoto kukua katika utimilifu wake.
No comments