HALMASHAURI NCHINI ZATAKIWA KUTENGA BAJETI YA PJT-MMMAM
Na Tonny Alphonce, Dodoma
Waziri wa Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt Doroth Gwajima
amewataka wakurugenzi wote wa halmashauri nchini kuhakikisha wanapata bajeti ya
kutekeleza Mpango wa Taifa wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto.
Dkt Gwajima
ameyasema hayo leo tarehe 11/12/2023 mjini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano
wa kitaifa wa wadau watekelezaji wa Program Jumuishi ya kitaifa ya malezi,
makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.
Amesema programu
hiyo ni muhimu kwa ukuaji timilifu wa mtoto na mkurugenzi atakayeshindwa kupata
bajeti hiyo atakuwa anachangia sababu zinazoweza kusababisha mtoto asiweze
kukua katika utimilifu wake.
Akizungumzia
mkutano mkubwa wa maelezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto unaotarajiwa
kufanyika mwezi wa tatu mwakani Dkt Ngwajima amewataka wadau wote wa afua za
watoto wajiandae vema ili washiriki kutoka nchi za afrika mashariki waweze
kujifunza kutoka Tanzania.
Awali akimkaribisha
mgeni rasimi mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya waatoto kutoka wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee, Wanawake na Makundi Maalumu Sebastian Kitiku amesema katika kuhakikisha
maeneo matano ya ECD yanafanyiwa kazi ambayo ni Lishe, Afya Bora, Malezi yenye
Mwitikio, Elimu na Ulinzi na Usalama wa Mtoto kwa uwiano wizara inampango wa
kuanza kupima maeneo hayo kwa Score Card.
“Mheshimiwa
Waziri hii Score Card itatusaidia kuhakikisha maeneo yote haya matano
yanatekelezwa kwa uwiano sawa na kwa kufanya hivyo ni wazi kuwa mtoto atakua
katika utimilifu wake”.alisema Mh Kitiku
Naye mkurugenzi mkazi kutoka Childrens in Crossfire Craig Ferla amesema hadi hivi sasa kuna maendeleo makubwa yameishapigwa katika halmashauri 114 tayari halmashauri 70 zimefikiwana programu hii.
Craig ameiomba pia serikali kuangalia namna ya kupata bajeti itakayosaidia utekelezaji wa programu hii kwa kasi.
kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa The Union Of Tanzania Press Clubs (UTPC) Kenneth Simbaya amewataka wadau wa watoto kwa pamoja kuwatumia waandishi wa habari katika shughuli zao ili kuipa jamii haki ya kupata habari.
Mkutano huu wa kitaifa wa wadau watekelezaji wa Program Jumuishi ya kitaifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ambao umewakutanisha Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Viongozi wa CSOs na Waandishi Vinara wa habari za watoto umeanza leo tarehe 11/12/2023 na Utamalizika tarehe 14/12/2023 mjini Dodoma ukiwa na lengo la kufanya tathimini ya Programu hii pamoja na kuzindua mpango maalumu wa utekelezaji wa programu hii.
No comments