BETWAY YAGAWA VIFAA VYA MICHEZO MBAGALA, YAPANIA KUKUZA SOKA LA TANZANIA KUANZIA NGAZI YA MTAA
Kampuni ya michezo ya kubashiri ya kimataifa, Betway Tanzania imeendeleza programu yake ya kutoa vifaa vya michezo kwa timu za soka za mtaani. Programu hiyo iliyozinduliwa Machi 2022 imelenga kusaidia maendeleo ya michezo nchini Tanzania kwa kutoa vifaa kwa timu za soka ngazi ya chini kabisa. Kupitia programu hiyo timu za mtaani hukabidhiwa mipira, jezi pamoja na soksi. Baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo timu hizo hushindana katika michezo ya mtaani maarufu kama ‘Kombe la Mbuzi’ ambapo mshindi hukabidhiwa mbuzi kama zawadi.
Mwishoni wa Novemba mwaka huu, Betway iligawa vifaa na kuendesha mashindano ya Kombe la Mbuzi yaliyoshirikisha timu nne za Mbagala Zakhiem wilaya ya Temeke, jijini Dare es Salaam. Timu zilizopata vifaa hivyo na kuingia katika michuano ya Kombe la Mbuzi ni Mizozo FC, Mnarani FC, Wajuba FC, na Mtoni Boys FC. Wajuba FC waliibuka washindi wa jumla na kupata zawadi ya mbuzi wawili baada ya kuifunga Mtoni Boys kwa 2-1.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vilivyofanyika Mbagala Zakhiem, Calvin Mhina, Afisa Masoko wa kampuni ya Betway Tanzania alieleza nia ya kampuni hiyo kuendelea kutoa mchango wake katika sekta ya michezo nchini kwa kuendesha programu mbalimbali zenye manufaa kwa wananchi ikiwemo program ya kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mtaani. Mhina alisisitiza kwamba mwendelezo wa pgoramu hii pia umetokana na mrejesho mzuri uliotolewa na wadau wakati na baada ya uzinduzi uliofanyika Tegeta, Dar es Salaam mwaka jana.
“Leo tuko hapa Mbagala na tunafuraha kuona wanamichezo na wakazi wa Mbagala wanafurahia kupata vifaa hivi kama ambavyo wanamichezo wa Tegeta walifurahia wakati tunazindua program hii mwaka jana. Hii ndio furaha yetu Betway Tanzania kuona programu zetu zikiongeza thamani kwa wanamichezo na sekta ya michezo kwa ujumla” ,amesema Mhina.
Afisa Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe amebainisha kuwa uamuzi wa kampuni hiyo kuangazia soka la mtaani ni sehemu ya Betway Tanzania kutoa mchango wake kwa jamii na kuchangia katika kukuza maendeleo ya sekta ya michezo nchini Tanzania.
"Programu hii inaitwa Kits for Africa katika ngazi ya bara la Afrika. Katika programu hii Betway inatoa vifaa kwa timu za mtaani ili kusisimua michezo katika ngazi ya chini kabisa kwani huko ndiko ambako vipaji vinakozaliwa. Kwa hapa Tanzania, programu hii pia itakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza thamani ya michezo katika ngazi za mitaa. Tumeamua kwenda kufanya zoeozi la kugawa vifaa katika vibanda vya kuonesha michezo maarufu kama vibanda umiza na kufanya mashindano ya Kombe la Mbuzi katika viwanja vya mtaani kabisa ili kugusa vipaji vya mtaani moja kwa moja”, amesema Masaoe.
Kwa upande wa timu zilizopata vifaa hivyo, nahodha wa Wajuba FC, aliipongeza Betway Tanzania kwa mpango wake huo, na kusema kuwa itaamsha ari ya wanamichezo mitaani na kurudisha hamasa ya vijana kushiriki michezo katika ngazi za mitaa.
"Mara nyingi timu zetu za mtaani huwa tunajichanga ili kupata vifaa kama jezi tunapotakiwa kushiriki mashindano ya mtaani. Mara nyingi kutokana na uhalisia wa maisha imekuwa vigumu kupata kiasi cha kutosha kununua vifaa vyenye ubora kama vilivyotolewa na Betway nah ii imekuwa kikwazo kikubwa kwa wengi wanaopenda michezo kushiriki mashindano mbalimbali. Najua hii kwangu binafsi na kwa timu zote zilizopata vifaa siku ya leo itachochea ushiriki wetu kwenye michezo”, amesema.
No comments