Breaking News

BARRICK BUZWAGI YAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUJITEGEMEA WILAYANI KAHAMA

   

Wanawake wa kikundi cha Busabi wakionyesha furaha ya kukabidhiwa mradi kwa kucheza kwa furaha pamoja na Wafanyakazi wa Barrick Buzwagi.

Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Kahama Richard Hegera, (katikati) na Wafanyakazi wa Barrick Buzwagi, wakiangalia maendeleo ya mradi wa ufugaji kuku wa mayai kabla ya mgodi huo kuukabidhi kwa kikundi cha Wanawake cha Busabi kilichopo Kahama katika hafla iliyofanyika kijijini hapo.
Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Kahama Richard Hegera, (katikati) na Wafanyakazi wa Barrick Buzwagi, wakiangalia maendeleo ya mradi wa ufugaji kuku wa mayai kabla ya mgodi huo kuukabidhi kwa kikundi cha Wanawake cha Busabi kilichopo Kahama katika hafla iliyofanyika kijijini hapo.
Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Kahama Richard Hegera, akiongea katika hafla ya Barrick Buzwagi kukabidhi mradi wa kujitegemea wa ufugaji kuku wa mayai kwa Kikundi cha Wanawake cha Busabi, kilichopo katika kata ya Mondo, wilayani Kahama jana,Wengine pichani ni Wafanyakazi wa mgodi huo.
Meneja wa Mgodi wa Barrick Buzwagi .Rebecca Stephen, akiongea katika hafla hiyo
Wanawake wa kikundi cha Busabi na wageni waalikwa wakifuatilia matukio katika hafla hiyo
***

Katika mwendelezo wake wa kuwawezesha wakazi wa maeneo yaliyopo jirani na Mgodi wa Barrick Buzwagi kuwa endelevu baada ya mgodi huo ambao uko katika mchakato wa kufungwa, Kikundi cha Wanawake cha Busabi, kilichopo katika kata ya Mondo, wilayani Kahama wamekabidhiwa mradi wa kisasa wa ufugaji kuku wa mayai.


Meneja wa Mgodi wa Buzwagi Bi. Rebecca Stephen, amesema utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya miradi iliyopo katika mpango wa kufunga mgodi wenye lengo la kuwawezesha wanawake na vijana kuwa na maisha endelevu kwa kuwa wengi wao walitegemea kuendesha maisha yao kwa kutegemea uwepo wa mgodi huo.


Alisema pamoja na kuwezesha kikundi hicho kupata mtaji pia wanakikundi wamewezeshwa kupata mafunzo ya vitendo na nadharia ya ufugaji kuku kwa njia ya kisasa na kimeunganishwa na soko la moja kwa moja la ndani ya mgodi huo kwa kuanzia ili kianze kunufaika na mradi huo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo , Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Kahama Richard Hegera, Barrick Buzwagi, kwa kuchukua hatua hiyo na kwamba mradi huo utasaidia kubadilisha maisha ya familia za wanakikundi hao pamoja na taifa kwa ujumla.

Aliwaasa walengwa wa mradi huo kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii kwa kutumia utaalamu wa kufuga kuku waliopatiwa ili mradi uweze kusimama na kuwa endelevu na kuleta manufaa yaliyokusudiwa.

Kwa upande wanakikundi hicho, wameushukuru Mgodi wa Buzwagi, kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo wanaamini yatawasaidia kuimarisha uchumi wao na taifa kwa ujumla.

No comments