WATUMISHI WA TCAA WAPONGEZWA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA wakati wa kufungua kikao hicho. Kulia ni Bi. Massa K. Mumburi Katibu Msaidizi wa Baraza, Kushoto ni Katibu wa Baraza Bw. Dedacus Mweya
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula akitoa pongezi wakati wa kikao cha Baraza
Katibu wa Baraza Bw. Mweya Dedacus akiwasilisha mrejesho wakati wa Baraza
Afisa Uchunguzi, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Bw. Silvanus Njenga akiwasilisha mada kuhusu Maadili ya Utumishi wa Umma
Menejimenti ya TCAA ikifuatia wasilisho la maadili.
Wajumbe wa Baraza wakiendelea kufuatilia mada hiyo
Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wamepongezwa kwa kuendelea kufanya Baraza la Wafanyakazi lenye tija lililofanya mamuzi makubwa yenye tija kwa kutuoa huduma bora na kukuza sekta ya usafiri wa anga nchini.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la TCAA uliofanyika Novemba 23,2023 makao makuu ya Mamlaka Banana jijini Dar es salaam.
Bw. Johari amewasifu wajumbe wa baraza kwa kufanya kuweka mbele maslahi ya taasisi na kuwasilisha hoja zinazoichochea menejimenti kutekeleza majukumu yake vyema. Pia ameongeza kuwa vikao hivyo vya Baraza ni njia bora ya kuimarisha demokrasia mahala pa kazi,na kuwataka wajumbe wa Baraza hilo kurudisha mrejesho kwa watumishi wenzao.
”Kama tunavyofahamu Mamlaka imetekeleza na inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ukiwemo wa Ununuzi wa Rada nne za kuongozea ndege, kuboresha Mfumo wa Masafa ya Mawasiliano wa Sauti baina ya rubani na waongozaji ndege katika vituo vyote vya kuongozea ndege nchini na Mradi wa kuimarisha na kuboresha utoaji taarifa za anga kuwa dijitali na yote hii ni mazao ya mawazo na hoja muhimu mnazoleta hapa na kwa pamoja tunapata ufumbuzi” alisema Bw. Johari.
Awali akiwasilisha salamu kwa niaba ya Chama cha Wafanyakazi Mkoa wa Dar es Salaam (TUGHE) Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kwa kuteleza majukumu yake kwa namna shirikishi kwani inafanya kila mtumishi kujisikia sehemu ya Mamlaka na hivyo kuongeza ari ya utendaji kazi.
Akitoa maelezo ya jumla, Katibu wa Baraza hilo Bw. Mweya Dedacus amesema hiki ni kikao cha sita cha Baraza ambacho dhima kuu ni kuwasilisha mrejesho wa yale yaliyokuwa yamejadiliwa na kuazimiwa wakati wa kikao kilichopita cha Baraza kilichofanyika mwezi Aprili.
No comments