MPC IMEFANYA UCHAGUZI KUJAZA NAFASI ZA VIONGOZI ZILIZOKUA WAZI
Na Mwandishi wetu, Mwanza.
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) imefanya uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi zilizokuwa wazi
Katika uchaguzi huo, nafasi zilizokuwa wazi ni pamoja na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na nafasi moja ya Mjumbe wa Kamati Tendaji huku jumla ya wanachama watano wakijitokeza kuwania nafasi hizo.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa MPC, wagombea alikuwa ni Debora Mallaba na Zefania Mandia ambapo Mallaba ameibuka mshindi kwa kupata kura 19 kati ya 24 zilizopigwa na wajumbe huku mpinzani wake, Mandia akipata kura tano.
Kwa upande wa Katibu Mkuu, Mgongo Kaitira ameibuka mshindi kwa kupata kura 17 kati ya 24 zilizopigwa huku dhidi ya Blandina Aristides aliyepata kura 7.
Nafasi ya mjumbe imechukuliwa na Kwilasa Mahingu ambaye kutokana na kutokuwa na upinzani amepigiwa kura 21 za 'Ndiyo' huku akipata kura tatu za 'Hapana'.
Baada ya uchaguzi huo, Kamati ya Uchaguzi huo wa dharura, iliyoongozwa na Jimmy Luhende na Abela Musikula imemtangaza Deborah Malaba kuwa Makamu Mwenyekiti wa MPC, Mgongo Kaitira (Katibu Mkuu wa MPC), na Kwilasa Mahingu kuwa Mjumbe wa MPC.
Picha mbalimbali za matukio ya Mkutano maalumu wa wa MPC wa kujaza nafasi za Viongozi zilizokua wazi.
No comments