MKUTANO WA KIDUNIA WA GEO WEEK 2023 WATAKA TAKWIMU ZAIDI ZITUMIKE KWENYE KUILINDA DUNIA
Na Edwin Soko,Afrika Kusini
Ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano wa Kidunia wa GEO WEEK unaoandaliwa na GEO Group on Earth Observations unaendelea hapa Capetown Afrika ya kusini, mkutano huo umezitaka serikali mbalimbali Duniani kutoa takwimu za uhalibifu wa Dunia ili kuonyesha ukubwa wa tatizo la uhalifu wa Dunia unaofanywa na wadau wa kimaendeleo.
Wanachama wa GEO WEEK ambao ni Nchi mbalimbali Duniani zimejielekeza kwenye kutumia sayansi na teknolojia zikiwemo satellite katika sekta zote kupata taarifa sahihi za uhalibifu wa Dunia ili zitumike kwenye kutatua changamoto za uhalibifu huo.
Nini maana ya GEO Group on Earth Observation ?
Hii ni jamii yenye wajibu wa kuilinda Dunia isipatwe na athari zinazoweza kuipoteza na kupoteza viumbe akiwemo mwanadanu, hivyo inajisimamia kupitia muungano wa Serikali za Nchi mbalimbali na kuwa na nguvu ya pamoja ya kuamua mustakabali wowote wa kuilinda Dunia.
Urusi, Marekani, Canada , ufaransa, UN na umoja wa ulaya zimeongoza ajenda ya uwekezaji kwenye sekta ya sayansi na teknolojia ili kupata suluhisho la kuilinda Dunia.
Pia wakuu wa Nchi mbalimbali Duniani wamesaini makubaliano maalmu ya kuchukua hatua kwenye kuilinda Dunia na kuifanya kuwa sehemu salama.
Wanachama wa GEO WEEK wamezitaka AZAKI na vyombo vya habari ziwe wabia kwenye mapambano ya kuilinda Dunia na kuifanya kuwa sehemu salama.
Mkutano huo pia ulitumia jukwaa la Mwaka huu 2023 kuzindua ripoti mbalimbali za mkutano wa Mwaka jana 2023 uliofanyika Jijini Acrra Ghana na kuja na mikakati ya maazimio ya Mwaka 2023.
Ministerail Summit
Katika mkutano wa Mwaka huu pia kuna vikao maalumu vya delegation za Serikali mbalimbali Duniani ambazo zina wajibu wa kukubaliana na maazimio na kurudi kuyatengenezea sheria kwenye Nchi husika.
Pia Nchi za Trinidaf na tabaco wamepitushwa na kuwa wanachama wapya wa GEO Group on Earth Observations kwa mwaka 2023.
Mkutano huu una umuhimu mkubwa kwa Nchi kama Tanzania kwa kupitia kubadilishana uzoefu, kunufaika na teknolojia pamoja na matumizi ya takwimu zinazokusanywa na GEO Community kwenye kutatua changamoto za uhalibifu wa Dunia katika sekta mbalimbali kama uvuvi, mifugo na nyinginezo .
Mkutano huo pia umepambwa na maonyesho ya sayansi na teknolojia kama uvumbuzi na ugunduzi wa satellite na vifaa mbalimbali vya kiteknolojia, ununuaji wa vifaa vya kisasa kama satellite na vinginevyo ambavyo ni zao la kukua kea teknolojia.
Nini cha kujifunza kwetu kama waandishi wa habari?
Uandishi wa habari umekuwa sana na teknojia inatupa nafasi ya kufanya ubobezi katika nyanja nyingi zaidi, mfano katika mkutano huu kuna dokezo la Digital Earth huu ni ubobezi wa kutumia sayansi kwenye kuijua na kuchunguza Dunia na kuandika habari za Ulinzi na usalama wa Dunia.
Hilo ni eneo la mfano tu lakini yapo maeneo mengine kama akili bandia kwenye kilimo, utafiti, afya na maeneo mengine..
Pia ni namna ya kutumia ushahidi jadidi / evidence based solution kwenye kutengeneza maudhui ya habari zetu pamoja na matumizi ya takwimu kwenye kuongea kwa ushahidi/ data use.
Nini cha kujifunza kama AZAKI?
Kuwa mdau muhimu wa kuibua changamoto za uhalibifu wa Kidunia na kufanya uchechemuzi wa kisera na kisheria kwenye kuilinda Dunia.
Pia kuona fursa katika mlengo adimu wa kuwa na mashirika yenye malengo ya kuilinda Dunia badala ya kuemdelea na maeneo ya kawaida kama haki za watoto na nyinginezo huku haki mtambuka ya kuwa na Dunia salama ikiachwa
Washiriki zaidi wa 2000 wameshiriki mkutano huo wakitoka kwenye serikali za Nchi mbalimbali, AZAKI, vyuo vikuu, Vyombo vya habari na mashirika ya kimataifa na kufanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mkutano wa Capetown hapa Afrika Kusini
No comments