EDWIN SOKO AIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWA MWANACHAMA WA GROUP ON EARTH OBSERVATIONS ILI NCHI INUFAIKE NA TEKNOLOJIA
Edwin Soko
Na Mwandishi wetu
Mwandishi wa habari mkongwe Edwin Soko ameiomba Serikali ya Tanzania kujiunga uanachama wa Group on Earth Observations ili iweze kunufaika na utumiaji wa sayansi na teknolojia kwenye kuilinda Dunia.
Soko amesema hayo alipofanya mahojiano kwa njia ya simu toka katika Jiji la Captown, Afrika Kusini alipokuwa akihudhuria mkutano wa GEO WEEK 2023 ambao unaandaliwa kila Mwaka na wanachama wa Group on Earth Observations ukiwa na lengo la kujadili matumizi ya sayansi na teknolojia kwenye kuilinda Dunia.
" Tanzania sio mwanachama wa Group on Earth Observations hivyo naiomba Nchi yangu kufanya tafakari ya kina juu ya umuhimu wa kuwa mwanachama wa Group on Earth Observations ili iweze kunufaika na faida za kuwa mwanachama kwenye matumizi ya sayansi na teknologia kwenye kukabiliana na changamoto za uhalibifu wa Kidunia",amesema
Soko amesema anawasilisha ombi hilo kupitia kwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia inayoongozwa na Mhe. Nape Nnauye ili kuchangamkia fursa hiyo kama Nchi.
" Nimekuwa nikishiriki mkutano huu kila Mwaka na kuona fursa nyingi ambazo Tanzania tunaweza kunufaika nazo kupitia hamasa ya kukuza teknolojia na matumizi ya teknolojia kwenye sekta zote za uchumi",ameongeza Soko
Pia amebainisha Nchi majirani kama Kenya, Uganda na nyinginezo tayari ni wanachama.
Pia amezitaja fursa zinazoweza kupatikana Tanzania ikiwa mwanachama ni pamoja na kufanya tafiti za pamoja, matumizi ya satellite kwenye nyanja tofauti tofauti, kubadilishana uzoefu na pia Nchi kujulikana kimataifa kwenye matumizi ya teknojia kujikomboa na changamoto mbalimbali.
No comments