WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUTANGAZA UTALII KUPITIA MICHEZO, YAZIDI KUNG'ARA MASHINDANO YA KAMBA - SHIMIWI
Na Mwandishi Wetu, IRINGA.
Timu ya wanaume ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeibuka mshindi kwenye mchezo wa kamba kwenye mashindano ya Shirikishio la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mkoani Iringa.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Kapteni wa timu hiyo, Faraja Mmasa amesema ushindi uliopatikana umetokana na maandalizi mazuri ambayo yameisaidia timu hiyo kushinda kwa seti mbili kwa sifuri dhidi ya wapinzani wao TARURA.
"Nianze kwa kuupongeza uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Kwa namna ambavyo walituandaa toka maandalizi mpaka kutuwezesha kufika hapa na kushiriki . Timu imejiandaa vizuri na kama unavyoona leo tulikuwa tunacheza mechi dhidi ya TARURA na tumeshinda ushindi wa seti mbili kwa bila." Amesema Mmasa
Ameongeza kuwa timu hiyo ina uwezo wa kusonga mbele kwa hatua zinazofuata kwani wao kama wachezaji wamejipanga vizuri kushindana na hatimaye kusinda kwa hatua zinazofuata.
‘’ Timu ya Wizara ya Maliasili na Utalii tumeona ni timu ambayo ipo Kwa ajili ya ushindani. Tumejipa kuendelea kusonga mbele kuchukua kikombe " Aliongeza Mmasa.
Naye mchezaji wa timu hiyo Paul Shayo amesema, mashindano hayo yanayoendelea mkoani Iringa ni njia moja wapo ya kuutangaza utalii wa ndani na hivyo wanatumia fursa hiyo vilivyo kuhamasisha utalii wa ndani
Kwa upande wa mchezaji Chamganda Hamis amesema, kwa ushindi walioupata wanamshukuru Mungu kwani utawasaidia katika safari yao ya kuelekea kunyakua vikombe.
No comments