Breaking News

RAIS SAMIA AMWAGA MABILIONI YA FEDHA KILIMANJARO KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO; MBUNGE MALEKO AFUNGUKA

Na Mwandishi Wetu, KILIMANJARO

MBUNGE wa Vitimaalum Mkoa wa Kilimanjaro Ester Malleko, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuwa kinara wa maendeleo, Mama mlezi, Mzazi, na Mfariji wa wasio matumaini, kwa kutoa mabilioni ya fedha katika Mkoa huo na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Amebainisha hayo leo Oktoba 5, 2023 wakati akizungumza katika Mikutano mbalimbali na kukutana na makundi ya Wanakilimanjaro akielezea namna alivyokoshwa na Rais SAMIA katika kuwatumikia Watanzania na kuwaletea maendeleo.

Amesema katika Mkoa huo wa Kilimanjaro ndani ya Utawala wake Rais Samia, ametoa fedha nyingi ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, jambo ambalo wanajivunia kuwa na Rais mpenda maendeleo hapa nchini.

Aidha, amesema mbali na mambo mengi aliyofanya Mhe. Rais kukuza Utalii, Ujenzi Uwanja wa Ndege moshi, UjenI Barabara kwa viwango mbalimbali ikiwemo Lami, katika Sekta ya Afya Rais Samia ametoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 2.59 ambazo zimetumika kuboresha huduma za Afya katika Zahanati 35, na Vituo vya Afya katika Mkoa huo wa Kilimanjaro.

Pia, amesema Rais Samia hakuishia hapo akatoa tena Sh.bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya katika Halmashauri za Moshi Mjini, Mwanga, Hai, Siha na Rombo.

Amesema pia Rais Samia ametoa fedha Sh. Bilioni 7.9 kwa ajili ya ujenzi wa Majengo ya Hospitali katika wilaya zote saba mkoani Kilimanjaro.

“Mkoa wa Kilimanjaro tunampongeza Rais Samia kwa kutoa mabilioni ya fedha na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, kwa kweli Rais Samia ni Kinara wa Maendeleo na sisi tutaendelea kumuunga mkono katika utawala wake ili awatumikie Watanzania,”amesema Malleko.

 

Akizungumzia Sekta ya Elimu, amesema katika Mkoa huo wa Kilimanjaro ametoa Sh.bilioni 21 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya elimu na uhifadhi wa mazingira, kwa shule zote za Msingi na Sekondari, pamoja na kutoa Bilioni 6.3 fedha za mpango wa elimu bila malipo.

Amesema kwa upande wa Sekta ya Maji, ametoa Sh.bilioni 6.29 ambao zimetumika kukarabati miundombinu ya Maji, na kuongeza mtandao wa upatikanaji Majisafi na Salama hadi maeneo ya vijijini.

Pia amesema katika kupambana na umaskini na kuwezesha wananchi kiuchumi kupitia mpango wa TASAF, kwamba Jumla ya Kaya 41,108 wamepata Ruzuku huku walengwa 27,472 wamenufaika na Ajira za muda za mpango huo katika miradi 604 ambayo inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri zote Saba mkoani humo.

Mbunge huyo pia amewashukuru Viongozi wa Serikali na Chama pamoja na Wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro, kwa namna wanavyompatia ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku kama Mbunge, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao ili kusukuma guruduma la maendeleo mkoani humo na kwamba Watanzania wamuunge Mkono Mhe. Rais Samia wasimvunje moyo kwakuwa ana mapenzi, dhamira na nia njema ya kuipaisha Tanzania kimaendeleo na kutoa Rai kwa wanasiasa kuacha nongwa na fitina za kisiasa za kugombania madaraka badala yake wachape kazi, wajenge utu, uzalendo na uadilifu na kumuunga mkono Rais Samia na Serikali yake.

No comments