Breaking News

JINSI MAMA MJAMZITO ANAVYOWEZA KUMKINGA MTOTO KUPATA MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI

Na Hadija Omary,Lindi

Ini ni kiungo muhimu sana ndani ya miili yetu hufanya kazi zaidi ya 500 ambapo moja ya kazi ya Ini ni kuchuja na kuondoa sumu kwenye Damu.

Ini linaweza kupata shida na kuvimba na kusababisha homa ya Ini (Heptitis) kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo Matumizi ya Pombe kupita kiasi, sumu kwenye damu

Wataalamu wanaeleza kuwa moja ya njia za usambaaji wa homa hiyo ya Ini ni kutoka kwa Mama Kwenda kwa mtoto ambapo inaelezwa kuwa Mama aliye na Maambukizi ya Hepatitis B humuambukiza mtoto baada ya kujifungua.

Iwapo hamna juhudi za matibabu za mapema za kuzuia maambukizi kuna uwezekano wa hadi asilimia 90 kwa mama kumuambukiza Mtoto.

Kutokana na Tatizo hilo Mratibu wa Afya ya uzazi na mtoto Kutoka kituo cha Afya cha Mji kilichopo Manispaa ya Lindi Mkoani humo (LINDI MC)  Farida Ibrahimu anawashauri akina Mama kuwahi cliniki pindi wanapojihisi kuwa ni wajawazito ili waweze kupata chanjo ikiwemo ya homa ya  Ini pamoja na ushahuri wa afya ya uzazi ili kuepukana na changamoto za maradhi kwa watoto watakao jifungua.

Mratibu huyo alisema kwa mama kuwahi kliniki pindi tu anapojihisi kuwa ni mjamzito, kulingana na vipimo vya awali atakavyofanyiwa  ataweza kujua   kama anamaambukizi ya aina yoyote ambayo yanaweza kumuathili mtoto alie tumboni au la na hivyo kuweza kumlinda mtoto huyo kitaalam mpaka atakapo zaliwa.

“katika maeneo hatari zaidi duniani virusi vya hepatitis b (hbv) kwa kawaida usambazwa kupitia kwa mama kwenda  kwa mtoto wakati wa kujifungua  au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hususani nyakati za utotoni “iwapo hamna juhudi za kitiba za kuzuia maambukizi kuna uwezekano hadi asilimia 90 kwa mama alie na  maambukizi ya hepatitis b kumuambukiza mtoto wakati wa kujifungua”.

 

anasema kama ilivyo kwa virusi vya ukimwi virusi vya homa ya Ini  pia uambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate,jasho na mwingiliano wa damu ya mtu mwenye virusi hivyo hivyo endapo mama mjamzito  hatapata chanjo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya  ni rahisi  kwa  Mtoto atakae jifungua kupata maambukizi hayo.

 

kutoka kwenye taarifa ya tovuti ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine inaonyesha homa ya ini sawa na janga linaloua kimya kimya ambapo kulingana na takwimu za vifo duniani  inakadiliwa kirusi cha Ini aina ya B pekee  huua watu 600,000 kila mwaka.

kwa wastani watu Zaidi ya bilioni mbili, sawa na asilimia 33 ya watu wote ulimwenguni, wameambukizwa Virusi vya HBV, na wengi wao upona baada ya miezi michache. Huku watu milioni350 wakiendelea kuwa na virusi hivyo Mwilini ambapo wengi huishi bila dalili na kuendelea kuambukiza watu wengine .

katika maeneo ya Bara la Afrika ambapo Tanzania ikiwemo maambukizi ya virusi vya homa ya Ini Ndio sababu kuu ya shida kwenye  Ini. Virusi vya homa ya Ini vipo vya aina 5 (A,B,C,D, na E) ingawa aina mbili za Virusi hivyo ( B na C ) ndio sababu kuu ya Ugonjwa wa Homa ya Ini kusambaa kupitia Damu na Maji maji ya mwili.

Kuwahi kituo cha kutolea huduma za Afya mapema kwa mama mjamzito hasa yule mwenye maambukizi ya ugonjwa huu wa Ini pindi tu anaposikia ari ya uchungu ni mhuhimu ili wataalamu kuweza kufanya maandalizi ya awali kwa ajili ya kumkinga Mtoto atakaezaliwa kama anavyoeleza  Grecy Mrope muuguzi mkunga katika kituo hiko cha Afya cha Mji


Mrope anaeleza kuwa Mama mjamzito anaweza kumkinga Mtoto wake asipate ugonjwa huo ni pale wahudumu au wataalamu wanapompatia Mama Mjamzito huduma kipindi cha kujifungua,ikiwemo njia ya kawaida au ya upasuaji.

Mtoto akishazaliwa anatakiwa kupewa dozi ya heptitis b imanune globenn hbig ndani ya masaa 12 ili kumkinga na homa ya ini.

Huku akieleza kuwa dozi hiyo inatakiwa apewe mara tatu, ambapo dozi ya kwanza atapatiwa   ndani ya  masaa 12 tangu azaliwe, dozi ya pili baada ya miezi sita na dozi ya mwisho ni baada ya mwaka mmoja kupita tokea mtoto huyo azaliwe.

Shuwea Juma mkazi wa manispaa ya Lindi anasema kuwa pamoja na ugonjwa huo wa ini kuwa ni ugonjwa hatari lakini bado elimu ya kutosha kuhusiana na ugonjwa huo haijafika kwa wananchi ambapo anasema uwenda maambukizi yakaendelea kuenea kwa kukosa Elimu.

“ mimi nadhani Elimu izidi kutolewa zaidi kwa wananchi juu ya ugonjwa huu kupitia kwenye vyombo vya habari hata mbao za matangazo na hata mashuleni kama ilivyo kwa magonjwa mengine kama vile ukimwi na hata corona  ili wananchi  tuchukuwe taadhari  zaidi za ugonjwa huo. Alieleza Shuwea

Pamoja na ugonjwa huu kuwa hatari na virusi vyake kusambaa na kuambukiza Mtu mara 100 zaidi ya virusi vya UKIMWI kama ilivyoelezwa katika tovuti ya Hospitali ya Mkoa wa Lindi Sokoine bado Elimu juu ya Homa hiyo haijafikishwa vya kutosha

No comments