ILEMELA YAENDELEA KUTENGA FEDHA ZA LISHE KWAAJILI YA WATOTO
Na Tonny Alphonce,Mwanza
Mwaka wa
fedha 2022/2023 halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza kupitia idara ya
afya ilitenga kiasi cha shilingi milioni 85.8 kutoka mapato ya ndani kwaajili ya watoto walio chini ya umri
wa miaka mitano ili waweze kupata lishe.
katika
kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/2023 Januari – Machi utekelezaji wa shughuli za lishe katika
halmashauri ya Ilemela ulifikia asilimia 77.5
Taarifa hiyo
ya utekelezaji wa shughuli za lishe
katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/23 ulilenga kutekeleza shughuli mbalimbali
ambazo ni kutoa elimu ya lishe kwa wazazi/walezi katika kata tatu za
Nyamhongolo, Bugogwa na Ilemela, usimamizi shirikishi pamoja na uhakiki wa
ubora wa takwimu za viashiria vya lishe kwa vituo vya kutolea huduma za afya ya
mama na mtoto, ununuzi wa chakula dawa kwa ajili ya kutibu watoto wenye umri
chini ya miaka 5 wenye utapiamlo pamoja na shughuli nyingine.
Jitihada hizo
za kutokomeza Utapiamlo zimeendelea ambapo tarehe 13/10/2023 halmashauri ya
Manispaa ya Ilemela kupitia kitengo cha lishe imeanzisha zoezi la ugawaji wa
chakula lishe kwa watoto wenye utapiamlo mkali katika mitaa yote 171 inayounda
Manispaa hiyo.
Katika zoezi
hilo la ugawaji wa chakula lishe kwa watoto wanaoishi katika Manispaa ya
Ilemela lililongozwa na Bi Mariam Msengi ambae ni Katibu Tawala wa Wilaya ya
Ilemela katika Kituo cha Afya cha Buswelu amesema kuwa Manispaa ya Ilemela inaunga mkono juhudi
za serikali ya awamu ya sita za uboreshaji wa
huduma za lishe kwa kutoa fedha katika sekta hiyo kwa kutambua umuhimu
wa wananchi wote kuwa na lishe bora tangu wakiwa wadogo ili kuwa na nguvu kazi
imara katika ujenzi wa taifa.
Bi Mariam, amewapongeza pia wanaume wenye watoto waliofika katika kituo cha afya Buswelu kwa ajili ya kupata huduma za kliniki pamoja na kusikiliza elimu ya lishe huku akiwasihi kina baba waliopo nyumbani kuhamasika na kutenga muda wa kuwa na watoto wao.
"
Nawapongeza kina baba waliojitokeza hapa leo kuleta watoto wao kupata huduma za
kliniki na pia kusikiliza elimu ya lishe inayotolewa na wataalam ni kitu kizuri
na kinajenga upendo wa mtoto kwa wazazi wote wawili baba na mama”.alisema Bi
Mariam
Akiwasilisha taarifa ya hali ya lishe ya wilaya ya Ilemela Bi.Pili Kassim amesema Halmashauri imeendelea kutenga kiasi cha shilingi 1000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka 5 katika kuhakikisha watoto wote wanafikiwa kwa lengo la kupunguza na kutokomeza Utapiamlo na kuendelea kuhamasisha jamii kulima mazao yenye viini lishe kwa wingi ili kuimarisha afya zao.
Bwana na
Bibi Nzobana ni wakazi wa kata ya Kahama katika mtaa wa Buyombe wao
wanaipongeza serikali kwa kuanzisha utaratibu wa ugawaji wa chakula lishe kwa watoto sambamba na
utoaji wa elimu endelevu ya lishe kwa wananchi.
Hadi sasa kiasi
cha Shilingi Milioni 7.45 kimetumika kununua chakula lishe hicho ambacho
kimetolewa kwa watoto 40 wenye umri wa kuanzia miezi sita hadi miaka 5 wenye
utapiamlo mkali ambapo lengo ikiwa ni
kuwafikia watoto 100 kwa kila robo ya mwaka.
CREDIT: Manispaa ya Ilemela.
No comments