Breaking News

UZINDUZI WA PJT- MMMAM MWANZA,KATIBU TAWALA AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE LISHE YA WATOTO

 Na Tonny Alphonce,Mwanza


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg Blandya Elikana amewataka wazazi na walezi wahakikishe wanawekeza kwa watoto wao wenye umri wa mwaka 0 hadi miaka 8,umri ambao kitaalamu umeonekana ndio utakaomjenga mtoto na kuwa mtu tegemezi kwa familia na taifa kwa ujumla.

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg Blandya Elikana akizindua rasimi program Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali mtoto mkoani Mwanza.

Katibu Tawala Ndg Elikana ameyasema hayo leo tarehe 22/09/2023 katika uzinduzi wa program Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali mtoto iliyofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya za Mwanza.

"Serikali inatambua umuhimu wa kuwekeza katika lishe kwa maendeleo ya mtoto kwa kuwa lishe duni huzalisha magonjwa,lishe bora itasababisha watoto kuwa na afya njema hali ambayo itamsaidia kukua vizuri na kuwa na uwezo mzuri awapo shuleni".alisema Ndg Blandya Elikana.

Ndg Elikana pia amesisitiza juu ya ulinzi wa watoto kuanzia kwenye ngazi ya familia ili kuhakikisha mtoto anakuwa salama kuanzia nyumbani ili kumkinga na aina mbalimbali za ukatili ili atakapokuwa mtu mzima itamjenga kujiamini na kuwa mdadisi na kuwa tegemeo kwa familia na taifa.

Kwa upande wake Joel Mwakapala  mwakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum amesema kila bajeti itakayopatikana katika mkoa husika itatumika kuitekeleza programu hiyo ambayo katika makadirio yaliyofanywa itagharimu zaidi ya Bilioni 900 fedha ambazo zitatokana na michango ya wadau mbalimbali yakiwemo mashirika yanayotekeleza afua za watoto.

Joel Mwakapala  mwakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu akizungumzia sababu ya serikali kuanzisha program Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali mtoto.


No comments