SARATANI YA MACHO YATAJWA KUWA TISHIO KWA WATOTO
Na Tonny Alphonce,Mwanza
Saratani ya macho kwa watoto wenye umri wa miaka 2-8
imetajwa kuwa miongoni mwa saratani ambazo ni tishio kwa watoto wadogo hapa
nchini.
“Unaweza kujiuliza
kwanini watoto hawa hufariki dunia! watoto wengi wenye saratani ya macho
wanafikishwa hospitali wakiwa wamechelewa,wanafikishwa hospitali saratani ikiwa
imefika mbali sana”.alisema daktari Mgaya.
Akizungumzia dalili za
ugonjwa wa Saratani ya macho daktari Mgaya amesema saratani ya macho ina dalili
kama za mtoto wa jicho ambapo katikati ya jicho kunakuwa na kitu cheupe badala
ya rangi nyeusi.
“Unaweza ukagundua kama
mtoto wako anaugonjwa wa saratani kwa kumpima kwenye mwanga hafifu unaweza
kuona jicho la mtoto wako linang’aa kama jicho la Paka lakini pia kuna watoto
wengine hupata makengeza ukiona hivyo wewe kama mlezi mlete mtoto wako apatiwe
matibabu”.alisema Mgaya
Daktari Mgaya amesema
endapo mzazi atamfikisha mapema mtoto wake hospitali mapema anaweza kutibiwa na
kupona na akawataka wazazi kujenga tabia ya kupima afya za watoto wao mara kwa
mara kwa lengo kuangalia maendeleo ya afya zao.
Daktari Kashaigili
amesema saratani za watoto zipo za aina mbalimbali na katika kupatiwa matibabu
hupatiwa ya aina tatu,matibabu ya kemikali,matibabu ya mionzi au matibabu ya
upasuaji au akahitaji matibabu yote ya aina tatu inategemea na saratani
imefikia katika hatua ipi.
Amesema kwa nchi
zinazoendelea takwimu za kitabibu za kidunia zinaonyesha kuwa saratani za
watoto zinatibika kwa zaidi ya asilimia 85 huku hapa nchini saratani za watoto
zinatibiwa chini ya asilimia 20 na watoto wenye saratani karibia asilimia 80
hufariki dunia.
Jenita Octavian
mwenyeji wa Kigoma ambae kwa sasa anaishi mkoani Mwanza amesema mtoto wake
alianza kuvimba tumbo akampeleka hospitali akaambiwa ana UTI na wengine
walimwambia amerogwa ila baadae madaktari wa wilaya wakamshauri ampeleke mtoto
Bugando ambapo alipimwa na kukutwa na saratani ya figo na alipatiwa matibabu na kupona.
Saratani ni ugonjwa
ambao unaathiri watu wa rika na jinsia zote watoto, watu wazima, wanawake na
wanaume ambapo takwimu za Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC) na
Shirika la Afya Duniani (WHO), 2018 zinaeleza kwamba kila mwaka duniani kote
kunatokea wagonjwa wapya wanaokadiriwa kufikia milioni 18.1, na kati ya hao,
zaidi ya wagonjwa milioni 9.6 hufariki kutokana na ugonjwa wa saratani kila
mwaka ambao ni sawa na takribani asilimia 50.
kampeni ya wiki ya kuhamasisha na kujenga uelewa juu ya saratani
kwa watoto hufanyika kila mwaka septemba
mosi mpaka septemba 30 na mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo kila mtoto
mwenyewe saratani anastahili
fursa ya tiba.
No comments