MNKONDYA ATEMBELEA SHAMBA LA VANILLA KUNDUCHI
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni kubwa ya kilimo cha vanilla 'Vanilla International Limited', Simon Mnkondya amefika katika shamba la Vanilla lililopo Kunduchi Beach na kutoa mafunzo ya kilimo cha vanilla huku akilinadi zao hilo kuwa lina bei kuliko mazao yote na kusema Vanilla Tanzania imewahi kuuzwa kwa bei kubwa kuzidi mazao yote yanayolimwa Tanzania.
Kunduchi ni Beach ambayo imeonekana vanilla kufanya vizuri zaidi kuliko maeneo mengine ya Dar es salaam na hii ni baada ya kupata vanilla ndefu yenye urefu upatao mita 13.
Mnkondya amewaasa wananchi wa Dar es salaam wajaribu kuingia mtandaoni na kuona kwa nini Kampuni ya Vanilla International Limited inahamasisha sana ulimaji wa zao la vanilla.
Pia amewashauri wananchi wa Dar es salaam na miji mingine kujikita katika kilimo mjini cha Vanilla kwa maana inahitajika eneo dogo tu kuweza kupata pesa nyingi huku akitanabaisha kuwa vanilla ina uwezo wa kuishi mpaka miaka 60.
Naye Mtaalam wa shamba hilo la Kunduchi bwana Robert ameeleza jinsi vanilla ilivyokuwa kwa haraka akisema kila anapoamka asubuhi anakuta vanilla imeongezeka kwa takribani sentimeta 2 ambapo amekiri kuwa ukuaji huo unatokana na uwepo wa jotomaji kubwa la asilimia 85(Humidity).
Naye Meneja Wa Mashamba ya Vanilla Arusha Bi.Mariam Kessy amekiri kuwa Kunduchi vanilla imekuwa kwa haraka zaidi ya maeneo mengine nchini na hivyo kuwashauri wanawake wenzake wajikite katika kilimo cha vanilla kwa maana ni zao mkombozi hasa ukizingatia kuwa ni zao la pili kwa bei duniani ambapo huwa linafikia mpaka bei ya dola 500 ambayo ni takribani sawa na milioni moja ya kitanzania.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni kubwa ya kilimo cha vanilla 'Vanilla International Limited', Simon Mnkondya akiangalia vanilla katika shamba la Vanilla lililopo Kunduchi Beach
No comments