MKURUGENZI MKUU TCAA AKAGUA MABORESHO YA MRADI WA MNARA WA KUONGOZEA NDEGE UWANJA WA NDEGE MTWARA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari (wa kwanza kushoto) akiongoza timu ya TCAA na Wakala wa Majengo (TBA) katika ukaguzi mradi wa maboresho ya mnara wa kuongozea ndege unaoendelea katika Uwanja wa ndege Mtwara
Mhandisi Swalehe Nyenye kutoka TCAA akielezea mpango wa maboresho uliopo kwenye ramani ya ujenzi wa mnara huo
Timu ikiendelea kukagua hatua za mnara wa muda unaoendelea kujengwa uwanjani hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari ameongoza timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Wakala wa Majengo (TBA) katika ukaguzi wa mradi wa maboresho ya mnara wa kuongozea ndege unaoendelea katika Uwanja wa ndege Mtwara.
Mradi huo unahusisha vipengele viwili ikiwa ni kujenga mnara wa muda ambapo utaruhusu waongozaji ndege kuendelea na kazi wakati mnara wa sasa ukifanyiwa maboresho unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Novemba.
Huu ni muendelezo wa uboreshaji wa miundombinu unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha wataalamu wanatekeleza majukumu yao katika mazingira mazuri ya kazi.
No comments