MAKATIBU NA WENYEVITI WA UWT KAHAMA WATUA BUNGENI DODOMA
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Lucy Mayenga amewakabidhi Makatibu na Wenyeviti wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) wa Kata 112 kutoka wilaya ya Kahama shilingi milioni 11.2 kwa ajili ya programu ya kuongeza Marafiki wa Chama Cha Mapinduzi sambamba na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na nchi nzima.
Programu hiyo Imezinduliwa leo Alhamisi Septemba 7,2023 na Mhe. Lucy Mayenga Jijini Dodoma baada ya Makatibu na Wenyeviti wa UWT kutoka Kata 112 kutoka wilaya ya Kahama kuwasili Mkoani Dodoma kwa mwaliko wa Mhe. Lucy Mayenga ambapo wakiwa Jijini Dodoma Viongozi hao wamepata nafasi ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tukio la uzinduzi wa Programu hiyo pia limehudhuriwa na viongozi wengine wakiwemo Mbunge wa jimbo la Msalala, Mhe. Idd Kassim, Mbunge wa Jimbo la Kahama Mhe. Jumanne Kishimba, Mbunge wa jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Viti Maalum Chadema Mhe. Salome Makamba, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ,Mbunge wa Viti Maalum Mtwara Mhe. Agnes Hokororo na Mbunge wa jimbo la Nyang'wale Mhe. Hussein Nassor.
No comments