TAMKO LA KULAANI KUSHAMBULIWA KWA WAANDISHI WA HABARI
Tukio hilo lilihusishwa kujeruhiwa kwa Waandishi wa habari wafuatao, Ferdnand Shayo (ITV), Dennis Msacky (Media Brain),Habib Mchange (Jamvi la Habari),Elia Kinian (Channel Ten),Janeth Joseph (Mwananchi), Dickson Busagaga (Clouds Media) na Mkalimani wao Lengai Ngoishiye,
Waandishi hao walikutwa na madhila hayo wakati wakitekeleza majukumu yao ya kikazi ya kutafuta taarifa za wamasai wanaoishi Ngorongoro na kutaka kuhama kwa hiari yao toka Kijiji cha Enduleni kilichopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
OJADACT inaamini kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha pamoja na Mamlaka nyingine za ulinzi na usalama zitawatafuta na kuwakamata watuhumiwa wa tukio hilo na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria ili wawajibishwe na iwe funzo kwa watu wengine wenye nia ovu dhidi ya waandishi wa habari.
Pia OJADACT inawakumbusha waandishi wa habari na vyombo vya habari kufanya tathimini ya ulinzi na usalama wa maeneo wanayotakiwa kwenda kufanya kazi zao ili kupungunza madhila yanayoweza kuwapata na pia OJADACT inatia pole majeruhi wote.
Edwin Soko
Mwenyekiti, OJADACT
Julai Agosti 17, 2023
No comments