ASILIMIA 75 YA WATOTO WANAOZALIWA UTUMBO UKIWA NJE HUFARIKI DUNIA
Na Tonny Alphonce, Mwanza
Akizungumzia tatizo
hilo mkurugenzi mkuu wa hospitali ya Bugando Fabian Masaga amesema tangu
Bugando ianze kutoa matibabu ya watoto wanaozaliwa utumbo nje ni asilimia 15 tu
ya watoto wanaopokelewa katikati hospitali ya Bugando hutibiwa na kupona huku
asilimia 75 hufariki dunia.
‘Tunaposema asilimia 15 ni ndogo kwasababu
ile asilimia 75 ya hawa watoto tunawapoteza kwa kweli ni uchungu kama ambavyo
tulivyoona baadhi ya kina mama hapa wakiongea kwa uchungu wakati wa kutoa
shuhuda’.alisema Masaga.
Masaga
amesema yawezekana baadhi ya watu wasijue ukubwa wa ugojwa huo lakini
kiuhalisia mtoto huzaliwa sehemu ya tumbo ya juu kwenye kitovu ikiwa wazi huku
ngozi yote huwa haipo na utumbo wote hutoka nje hali ambayo inatisha na endapo mtoto atacheleweshewa matibabu ni wazi kuwa anaweza kufariki dunia.
Masaga amesema
takwimu za kidunia zinaonyesha kuwa kati ya watoto 4000 wanaozaliwa mmoja
hukutwa na tatizo hilo na kwa Bugando takwimu zinaonyesha kwa wastani kwa mwaka
mzima wanapokea watoto 290 sawa na
watoto 10 kwa mwezi huku kwa wiki ni sawa na watoto watatu hadi watano
wanapokelewa hali ambayo inaashiria
tatizo hili ni kubwa.
Kwa upande
wake Daktari Sister Alicia Masinga
kutoka kitengo cha upasuaji wa watoto Bugando amesema ili kupunguza vifo vya watoto
wanaozaliwa wakiwa na utumbo nje wamama wajawazito walio chini ya umri wa miaka 25 wanatakiwa kufanya
kipimo cha Utra Sound kwasababu katika umri huo kuna uwezekano wa wao kuzaa
mtoto mwenye changamoto hiyo.
Sister Masinga amesema hatua nyingine kwa mama endapo atagundulika kuwa na mtoto mwenye utumbo nje anatakiwa kujifungulia katika hospitali inayotoa huduma ya watoto hao kwasababu matibabu huanza mara moja baada ya mtoto kuzaliwa ili kuokoa maisha ya mtoto na kuongeza kuwa kwa sasa hospitali zinazotoa huduma hiyo kwa sasa ni Bugando na Muhimbili.
‘Ukiangalia sababu zisizo rasimi za
tatizo hili inawezekana likawa linasababishwa na mabinti wanashika ujauzito
wakiwa na umri mdogo kwa sababu tafiti zimewabaini wanaojifungua watoto wakiwa
utumbo nje wengi wao umri wao ni chini ya miaka 25’.alisema Sister Msinga
Akizungumzia
majukumu wanayotakiwa kufanya wahudumu wa afya mara baada ya kuwapata watoto
waliozaliwa utumbo nje sister Masinga amesema ni vema wakawasiliana na
hospitali ya Bugando au Muhimbili ili wapewa maelekezo ya namna gani ya kuwapa
huduma ya kwanza watoto hao itakayowawezesha kufika salama Bugando au Muhimbili
kwaajili ya matibabu.
‘Wakiapata huduma ya kwanza
inayopaswa hata wakicheleweshwa inasaidia hawa watoto kufika Bugando wakiwa na
hali nzuri na watapatiwa matibabu na kuokoa maisha yao’.alisema Sister Masinga
Jesca James
kutoka mkoani Geita ambae alijifungua mtoto ambae utumbo ukiwa nje anasema alijisikia
vibaya mara baada ya kujifungua na kugundua kuwa mtoto wake anashida hiyo
lakini mtoto alipatiwa matibabu na kupona baada ya miezi miwili.
Jesca amesema
majirani baada ya kugundua kuwa amejifungua mtoto akiwa na utumbo nje
walimkatisha tamaa kwa kusema kuwa mtoto huyo lazima atakufa lakini hakukata tamaa
na kumpeleka Bugando kwa matibabu na akapona.
Naye Reticia
Adam kutoka mkoani Kagera amesema alipojifungua mtoto mwenye tatizo hilo la utumbo
wazi lilimshangaza hadi daktari aliyemzalisha kwasababu ilikuwa ni mara yake ya
kwanza kushuhudia mama akijifungua mtoto mwenye tatizo hilo.
Nao wadau wa
Afya Judith Nashon mwanasheria kutoka
shirika la Railway Children Afrika na mkurugenzi wa Desk and Chair Foundation
Sibtain Meghji wamesema wataendelea kutoa msaada kwa hospitali ya Bugando pale
watakapo lazimika kufanya hivyo kwa lengo la kuokoa maisha ya watoto
wanaokumbwa na changamoto mbalimbali za afya.
Mwanasheria kutoka shirika la Railway Children Afrika Judith Nashon akizungumza namna shirika lao linavyoshirikiana na hospitali ya Bugando katika masuala ya afya kwa watoto.
Hadi hivi sasa bado haifahamiki sababu hasa za mama kujifungua mtoto utumbo ukiwa nje japo tafiti mbalimbali bado zinaendelea kufanyika huku hospitali ya rufaa ya Bugando kupitia chuo chake cha afya nayo ikijipanga kuanza kufanya utafiti ili kujua chanzo cha tatizo hilo la mtoto kuzaliwa akiwa utumbo nje.
No comments