BENKI YA AZANIA YAHAMASISHA WANAWAKE KUCHANGAMKIA AKAUNTI YA HODARI
Afisa Mahusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Dorah Chacha akitoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa katika Benki hiyo ikiwemo Akaunti na Mikopo maalumu kwa ajili ya wanawake (Akaunti ya Mwanamke Hodari). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Mahusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Dorah Chacha akitoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa katika Benki hiyo ikiwemo Akaunti na Mikopo maalumu kwa ajili ya wanawake (Akaunti ya Hodari)
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya Azania imewahamasisha Wanawake Wajasirimali wakiwemo Mama Lishe kuchangamkia huduma zinazotolewa katika Benki hiyo kama vile Akaunti na Mkopo maalumu kwa ajili ya wanawake (Azania Bank Hodari) ili waweze kutimiza malengo yao.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Mahusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Dorah Chacha leo Jumatano Julai 5,2023 wakati wa mkutano wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga na Mama Lishe na Wajasiriamali wilayani Kahama ambapo Mbunge huyo ametoa msaada wa Majiko ya Gesi 250 kwa Mama Lishe Wilaya ya Kahama ili kuwarahishia kazi katika shughuli zao sambamba na utunzaji mazingira kwa kutumia nishati mbadala.
Afisa Mahusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Dorah Chacha amesema Akaunti na Mkopo Mahsusi kwa wanawake (Mwanamke Hodari) inafunguliwa bure, hakuna makato ya mwezi ,kutoa fedha dirishani ni bure na riba1% tu kwa mwezi.
"Mwanamke Hodari ni yule anayetimiza malengo kwa juhudi na mikakati maalum, mwanamke asiyekata tamaa, hufanya lolote zuri na lenye faida kutimiza malengo yake kibiashara ili kupata riziki. Hivyo Benki ya Azania inaungana nawe mwanamke hodari kwa kukutengenezea akaunti na mikopo sahihi kwa ajili yako wewe ambaye ni mwanamke wa kisasa, jasiri, imara unayejali maendeleo na mwenye maono ya kusimamia yale yanayonufaisha maisha yako na jamii inayokuzunguka. Karibuni sana Azania Benki ili mnufaike na Akaunti ya hodari ",amesema Dorah.
Amezitaja sifa za Akaunti ya Hodari kuwa ni akaunti inayofunguliwa bure bila kiwango cha kuanzia, hakuna makato ya mwezi, kutoa pesa dirishani bure, unapata kadi ya Visa (ATM) lakini pia Akaunti hiyo ina bima ya mazishi.
"Sifa za mikopo ya Hodari ni riba nafuu ya 1% tu kwa mwezi, mwanamke hodari ataweza kukopa mara nne ya akiba aliyoweka benki, dhamana ya 75% kutoka African Guarantee Fund (AGF). Pia Mkopo unaanzia shilingi 200,000/= mpaka 500,000,000/=",ameongeza Afisa Mahusiano huyo wa Benki ya Azania tawi la Kahama.
Afisa Mahusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Dorah Chacha akitoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa katika Benki hiyo ikiwemo Akaunti na Mikopo maalumu kwa ajili ya wanawake (Mwanamke Hodari). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Mahusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Dorah Chacha akimpatia Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kipeperushi kinachoelezea huduma maalumu kwa ajili ya wanawake zinazotolewa katika Benki ya Azania
Afisa Mahusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Dorah Chacha akimpatia Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita kipeperushi kinachoelezea huduma maalumu kwa ajili ya wanawake zinazotolewa katika Benki ya Azania
Afisa Mahusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Dorah Chacha akitoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa katika Benki hiyo ikiwemo Akaunti na Mikopo maalumu kwa ajili ya wanawake (Mwanamke Hodari)

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akizungumza na Mama Lishe na Wajasiriamali wilayani Kahama leo Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga akiangalia majiko 250 ya gesi kabla ya kuyakabidhi kwa Mama Lishe wilayani Kahama.
Muonekano wa sehemu ya majiko ya gesi yaliyotolewa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga kwa Mama Lishe wilayani Kahama

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Thomas Mayenga (kushoto) akikabidhi jiko la gesi kwa Mama Lishe wilayani Kahama
No comments