WAFANYAKAZI WA BARRICK NORTH MARA WALIVYOSHIRIKI MBIO ZA CAPITAL CITY MARATHON
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara, walioshiriki mbio za City Marathon wakifurahi pamoja baada ya kumaliza kukimbia.
Naibu Spika,Mh. Azzan Zungu (katikati) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara walioshiriki mbio za City Marathon
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara walioshiriki mbio za City Marathon katika picha ya pamoja ya kumaliza kukimbia
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kukimbia mbio za City Marathon, jijini Dodoma
****
Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara, uliopo wilayani Tarime, wameshiriki katika mbio za Capital city Marathon zilizofanyika Mkoani Dodoma ambapo wamemudu kukimbia mbio za masafa marefu.
Kampuni ya Barrick nchini imekuwa na program za mazoezi kwa ajili ya kuhakikisha wafanyakazi wake wanakuwa na nguvu na afya bora.
Kila mwaka kampuni imekuwa ikiwezesha wafanyakazi wake kushiriki mashindano mbalimbali ya michezo ikiwemo mashindano ya mbio za kilomita 42 ya Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon yanayofanyika kila mwaka.
No comments