OJADACT YAIPONGEZA SERIKALI MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA
Chama cha waandishi wa habari wa kupinga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania OJADACT kinaipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya kuthibiti na kupambana na dawa kulevya Nchini DCEA kwa kufanya kazi zake kwa weledi kwenye kupambana na dawa za kulevya Nchini.
Mwenyekiti wa OJADACT Edwin Soko amesema hayo leo kwenye maadhimisho ya siku ya kupambana na dawa za kulevya duniani na kuwataka vijana ambao ndiyo wanatajwa kuhusika na matumizi ya dawa hizo kuacha mara moja
"Kwa mwaka 2021 - 2022 vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa kwenye kutoa elimu ya madhara ya dawa za kulevya kupitia vyombo vya kale na vya kisasa na sisi
OJADACT tulisaidia kuwaunganisha wadau wa kupambana na dawa za kulevya na watangazaji wa programu za utoaji elimu ya athari za dawa za kulevya katika kuendelea kielimisha jamii juu madhara ya dawa hizo za kulevya na tunaendelea kuiomba serikali kuendelea
kuiwezesha mamlaka ya uthibiti na kupamba na dawa za lulevya ili iendelee kufanya kazi zake kiweledi"
Pia Somo amewapongeza wadau mbalimbali wakiwemo NSSF Mkoa wa Mwanza kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha vijana wanakua salama dhidi ya janga la dawa za kulevya.
"NSSF wamekuwa wadau muhimu kwetu kwani mara kwa mara wametuunga mkono OJADACT kwenye kutusaidia baadhi ya shughuli na mipango yetu kutekelezeka" Alisema Soko
,.................MWISHO..............
No comments