CFAO MOTORS TANZANIA KUSHIRIKIANA NA MAKAMPUNI YA NDANI KUSAMBAZA VIPURI HALISI VYA MAGARI MKOANI IRINGA NA MOROGORO
CFAO Motors, kampuni ya usambazaji magari na vifaa vya magari barani Afrika imeendela kutanua wigo nchini Tanzania kwa kufungua duka la Winpart mkoani Iringa na Morogoro. Kampuni hiyo inayojulikana zaidi kwa kusambaza magari mapya na vifaa halisi vya magari kutoka kwa wasambazaji imeshirikiana na kampuni za ndani kufungua matawi ya duka lake la uuzaji wa vifaa mikoani humo.
Matukio ya uzinduzi huo yaliyofanyika Iringa na Morogoro yamehudhuriwa na wawakilishi kutoka CFAO Motors Tanzania, TENS na Wheelerz. Uzinduzi wa WinPart katika mikoa hiyo unamaanisha kwamba watumiaji wa magari wa Iringa na Morogoro watapata vifaa halisi vya magari na kuwasaidia kuondokana na bughudha za matengenezo ya maghari yao mara kwa mara.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Wheelerz, Said Mohamed Sood, ambao ni wabia wenye wa CFAO Motors mkoani Iringa na Nyanda za Juu Kusini, akizungumza katika hafla hiyo amedhihirisha hitaji kubwa la vipuri vyenye ubora mkoani humo na mikoa ya jirani.
"Wateja wengi wanachangamoto ya kupata vipuri asili vya magari wakati magari yao yanapoharibika," alisema.
“Hivyo ushirikiano huu baina yetu na CFAO Motors Tanzania ambao wanatoa vipuri vya asili vya magari kupitia Winpart ni wa manufaa makubwa sana kwa wamiliki wa magari.” Aliongeza Said.
Kupitia ushirikiano na CFAO Motors Tanzania, Wheelerz na makampuni mengine ya ndani yataweza kupata vipuri asili moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji. Winpart iliyo chini ya CFAO Motors Tanzania ndio msambazaji pekee nchini Tanzania anayenunua vipuri vya magari moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji, na kuhakikisha kuwa wateja wanapata vipuri halisi.
Erca Uisso, Mratibu wa Masoko wa CFAO Motors Tanzania, naye alizungumza katika hafla hiyo, akisisitiza dhamira ya kampuni hiyo katika kusimamia ubora na uaminifu katika huduma zake.
"Tumekuwa tukifanya kazi kwa ushirikiano na TENS kwa miaka mingi. Wanajulikana kwa huduma zao bora na uaminifu hapa Morogoro na mikoa ya jirani," alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa TENS , Peter Ngowi pia alielezea kufurahishwa kwake na ushirikiano huo, akiita Winpart "mkombozi” ambaye utasaidia kuwapa wateja vipuri vyenye ubora vinavyodumu kwa muda mrefu na kuhakikisha magari yao yapo salama.
"Tumefurahishwa sana na ushirikiano huu kwa sababu CFAO Motors wameleta suluhisho hili kwa wamiliki wa magari mkoni Morogoro kupata vipuri vya magari vyenye ubora wa kimataifa na ambavyo vinadumu na kuhakikisha usalama wa mmiliki na mtumiaji wa gari”, Ngowi alisema.
Uzinduzi wa Winpart huko Iringa na Morogoro ni hatua muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa vipuri bora katika maeneo yote ya Tanzania kwa ujumla.
No comments