BARRICK BULYANHULU NA GGML WAONYESHANA UBABE MCHEZO WA KIRAFIKI WA BASKET BALL
Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya kutoka Barrick Bulyanhulu na GGML wakiwania mpira wakati wa mchezo huo wa kirafiki
Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya kutoka Barrick Bulyanhulu na GGML wakiwania mpira wakati wa mchezo huo wa kirafiki
Wachezaji wa GGML katika picha ya pamoja baada ya mechi hiyo ya kirafiki kumalizika
Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya kutoka Barrick Bulyanhulu na GGML wakiwania mpira wakati wa mchezo huo wa kirafiki
Wachezaji wa GGML wakipata mawaidha kutoka kwa kocha wao
Wachezaji wa Barrick Bulyanhulu wakipata mawaidha kutoka kwa kocha wao
Baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu wakifuatilia mchezo huo
****
Timu za mchezo wa kikapu za wafanyakazi kutoka migodi mikubwa ya dhahabu nchini ya Barrick Bulyanhulu na Geita Gold Mine Ltd. (GGML) zilionyeshana umwamba katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika viwanja vya michezo vya mgodi wa Bulyanhulu.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali GGML ilibuka na ushindi wa magoli 85 dhidi ya magoli 81 yaliyofungwa na timu ya Barrick Bulyanhulu.
Mchezo huo mbali na kudumisha urafiki na kuleta furaha ni mwendelezo wa programu za makampuni hayo ya kuhakikisha wafanyakazi wake wanafanya mazoezi ya kujenga afya zao.
Kampuni ya Barrick nchini imekuwa na program za mazoezi kwa ajili ya kuhakikisha wafanyakazi wake wanakuwa na nguvu na afya bora.
Kila mwaka kampuni imekuwa ikiwezesha wafanyakazi wake kushiriki mashindano mbalimbali ya michezo ikiwemo mashindano ya mbio za kilomita 42 ya Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon,
yanayofanyika kila mwaka.
No comments