SHIRIKA LA DWWT LATOA TUZO KWA WANAWAKE NA WASICHANA WAVIU
Tonny Alphonce,Dar es Salaam
Shirika la Dignit and wellbeing for women living
with hiv in Tanzania (DWWT) limeombwa kuendelea kuwatambua na kuwapa moyo wa
kufanyakazi kwa bidii wanawake na wasichana ambao wanapambana na changamoto za
UKIMWI nchini.
Kauli hiyo imetolewa na mratibu wa UKIMWI jijini Dar es Salaam
Grace Kessy ambae alikuwa mgeni rasimi katika sherehe za kuwapongeza na kuwapa tuzo za
F.I.E.R.C.E wanawake na wasichana WAVIU kutokana na mafanikio na kazi nyingi
walizofanya katika mwitikio wa VVIU na UKIMWI nchini.
Grace amesema mafanikio makubwa yameonekana kwa upande wa VVU na UKIMWI kutokana na jitihada na kazi
zinazofanywa na wanawake na wasichana katika jamii ya watanzania na kupelekea
watu wanaoishi na VVU kuwa na matumaini ya kuendelea kuishi na wengine
wakihamasika kupima afya zao.
“Tunatambua umuhimu wa ushirikiano kati ya
mashirika yasiyo ya kiserikali na leo napenda kuwashukuru DWWT kwa jitihada zao
za kipekee katika kuboresha afya na ustawi wa wanawake wanaoishi na VVU”.alisema
Grace
Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya DWWT Veronica Joseph amesema lengo la
kuanzishwa shirika la DWWT ni kuwajengea uwezo wanawake na wasichana WAVIU
katika kutetea na kukuza mahitaji na haki zao wenyewe pamoja na kuwa na jamii
inayoheshimu na kutoa ushirikiano wa upatikanaji wa haki na huduma kwa wanawake
na wasichana WAVIU katika ngazi zote.
“Tukio la leo ni ushahidi wa nguvu za
wanawake na wasichana katika mapambano ya VVU na UKIMWI katika Nyanja zote
kuanzia kinga,tiba na matunzo maeneo hayo mmeyafanyiakazi vilivyo na mnastahili
kupata tuzo hizi.”alisema Veronica
Nae Rustika Banzi ambaye ameshinda tuzo na
kupata nafasi ya kuiwakilisha DWWT nchini Uganda amewashukuru wale wote
waliompigia kura na kuibuka mshindi huku akitoa ahadi ya kuendelea kuwa saidia
WAVIU kuanzisha miradi ya kiuchumi pamoja na kuendelea kutoa elimu juu ya
umuhimu wa kutumia dawa za ARV kwa usahihi.
Utoaji wa tuzo hizo za F.I.E.R.C.E.
uliandaliwa na shirika la DWWT kwa udhamini wa Jumuiya ya kimataifa ya wanawake
waishio na VVU ukanda wa Afrika Mshariki (ICWEA) ka kutolewa katika ofisi za
NACOPHA makao makuu jijini Dar es Salaam tarehe 19/05/2023.
No comments