MISA TANZANIA YASHEREHEKEA MIAKA 30 TANGU KUANZISHWA KWAKE
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari- MAELEZO Gerson Msigwa akizunguza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Misa Tanzania leo Jijini Dodoma.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), imeadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 huku ikijivunia makubwa iliyoyafikia kwa kipindi hicho.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo Alhamisi Mei 25,2023 katika ukumbi wa New Dodoma Hotel Jijini Dodoma yakihudhuriwa na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari, pamoja na wanachama wa Misa Tanzania ambapo mgeni rasmi alikuwa Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari- MAELEZO Gerson Msigwa kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekonolojia ya Habari, Nape Nnauye.
Akizungumza wakati akifungua Maadhimisho ya Miaka 30 ya MISA Tanzania, Msigwa amesema Serikali kupitia Wizara ya habari Teknolojia na Mawasiliano itaendelea kushirikiana vyema na waandishi wa habari katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili pamoja na kutekeleza Maagizo ya Rais Samia ya kuifanyia Marekebisho ya Sheria ya huduma za habari ya mwaka (2016) kwa kurekebisha vifungu ambavyo vinabinya uhuru wa habari na kujieleza.
Amesema serikali inaendelea kuboresha mazingira ya vyombo vya habari huku akisisitiza kuwa tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani hakuna chombo kilichofungiwa na vilivyokuwa vimefungiwa vimefunguliwa.
“Serikali chini ya Rais Samia inatambua kazi nzuri inayofanywa na waandishi wa habari na ipo bega kwa bega na Waandishi wa habari na ndiyo maana ndani ya miaka miwili ya utawala wake hamjasikia chombo chochote cha habari ambacho kimefungiwa na Magazeti ambayo yalifungiwa yamefunguliwa”, amesema Msigwa.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari- MAELEZO Gerson Msigwa.
Msigwa pia amesema katika kipindi hiki mafunzo/semina kwa waandishi zinahitajika sana hivyo kuiomba Misa Tanzania na wadau wengine kuwapatia mafunzo mbalimbali waandishi wa habari.
"Katika kipindi hiki tunahitaji sana mafunzo kwa waandishi wa habari. Katika program zetu tuimarishe sana mafunzo kwa waandishi wa habari, Misa Tanzania na wadau wengine tutie mkazo sana kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari.Mimi ni miongoni mwa wanufaika wa mafunzo kwa wanahabari ambayo yamekuwa yakitolewa na taasisi ya habari ya MISA-Tanzania",amesema Msigwa.
Mwenyekiti wa Misa Tanzania, Salome Kitomari
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari amempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayofanya ya kuwatumikia Watanzania, lakini zaidi kwa namna amechukua hatua kadhaa zilizowezesha waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuondoa vikwazo vingi.
Amesema MISA Tanzania imepita kwenye safari ya miaka 30 yenye milima na mabonde na kutokana na mambo yote hayo ameupongeza uongozi, sekretarieti na wanachama wa MISA Tanzania kwa kushikamana mpaka kufikia hatua hiyo.
"Tuna mengi ya kujivunia ikiwemo kuwa na Ofisi yetu eneo la Kinondoni Mkwajuni, Dar es Salaam na kubaki kwenye DNA ya MISA ya Uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa taarifa nchini.Wanachama kutoka taasisi na mwanachama mmoja mmoja,Viongozi waliopita wenye mchango kubwa kwenye tasnia ya habari na Wadau wa Maendeleo kutoka serikali za Canada, Finland, Uingereza, Ujerumani, Marekani na nyinginezo",amesema Mwenyekiti huyo wa Misa Tanzania.
Amesema mafanikio mengine ni pamoja na kutoa mafunzo ya ndani na nje ya nchi kwa waandishi wa habari, Kuwezesha uanzishwaji wa vyombo vingine vya habari zikiwamo Radio za Kijamii na kufanya uragibishi kwenye sheria mbalimbali tangu Sheria ya Magazeti, Sheria ya Huduma za Habari, Sheria ya Haki ya Taarifa na nyinginezo.
"MISA Tanzania kwa kushirikiana na washirika wake imefanya mafunzo nchi nzima kuwajengea uwezo waandishi kuzijua sheria zinazosimamia taaluma lakini pia kuhakikisha upatikanaji wa taarifa kwa kusukuma kuwa na Sheria ya Haki ya Taarifa, 2016, na kuongeza msukumo wa utoaji wa taarifa. Mathalani, Kila mwaka Septemba 28, ambayo ni siku ya Haki ya Taarifa, MISA hutoa ripoti ya utafiti kuonyesha wale waliofanyiwa utafiti kwa kiasi gani walitoa taarifa.Kwa ujumla kuna mabadiliko siku hadi siku.Pia kukutana na wabunge, viongozi wa serikali",amesema Kitomari.
Pia Misa Tanzania imewawezasha waandishi kwenda kuandika habari za upatikanaji wa taarifa, sheria mbalimbali, habari za jinsia na COVID-19.
"Pamoja na mafanikio mengi miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili tasnia ya habari nchini ni pamoja na Uchumi wa wanahabari. Pamoja na kwamba ni wajibu wa waandishi wa habari kupasha habari kwa Watanzania lakini wengi wana hali ngumu kimaisha, hawana mikataba, bima za afya na stahiki nyingine za kisheria kama michango kwneye mifuko ya hifadhi ya jamii.Hali hii inaathari kubwa kwenye mchakato wa habari kwa kuwa kunatoa mwanya wa rushwa kwa sababu siku zote tumbo lenye haliwezeshi ubongo kufikiri vyema",amesema Kitomari.
"Tunashukuru serikali kwa hatua ilizochukua kwa kuunda Kamati ambayo tunaamini itakuja na suluhisho litakaloisaidia sekta ya habari kustawi wa sekta hii ambayo ina nafasi kubwa ya kuchangia pato la taifa",amesema.
"Kipekee na kwa umuhimu mkubwa nawashukuru wadau wetu (partiners) UNESCO, Internews, Fredirch Naumann Foundation for Freedom (FNF), Freedom House na USAID kwa kuendelea kushirikiana nasi bila kuchoka kuhakikisha ndoto yetu inatimia. Msaada wenu utaandikwa kwa wino usiofutika",ameongeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Misa Tanzania, Elizabeth Riziki amesema Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara,Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), inaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake,MISA Tanzania ilizaliwa mwaka 1993 baada ya kikao cha wanahabari waliokutana Windhoek, Namibia kujadili mambo mbalimbali yaliyokuwa yanaukabili Ukanda wa Nchi za Kusini.
"MISA ina matawi tisa katika nchi za Zambia, Msumbiji, Malawi, Lesotho, Botswana, Namibia, Angola, Tanzania na Zimbabwe ambako ndiyo makao makuu ya matawi yote.
Kwa mwaka huu, MISA Tanzania inaadhimisha miaka 30, MISA inafanya kazi ya kichechemuzi katika uhuru wa Habari, kupata na kutoa taarifa na uhuru wa kujieleza",amesema Riziki.
"Mwaka huu MISA inafanya maadhimisho hayo kwa kuangalia uchechemuzi wa uhuru wa kujieleza kama msingi wa haki zote na moja ya maeneo makuu ambayo MISA inafanyia kazi; kwa kuangalia namna ulivyokua ukifanyika, unavyofanyika na namna gani tufanye kuboresha kulingana na mabadiliko ya wakati na teknolojia"ameongeza.
Mkurugenzi wa Misa Tanzania, Elizabeth Riziki.
"MISA -Tanzania pamoja na wadau wa maendeleo wanaofanya uchechemuzi kwenye uhuru wa kujieleza walioalikwa kutoka makundi yote, Watoto, vijana, wanawake, watu wanaoishi na ulemavu, mashirika ya kidini, wadau wa maendeleo wa kimataifa na kitaifa watajadiliana na kuona namna gani tunaweza boresha mazingira ya uhuru wa kujieleza kwa jamii nzima. Namna gani tunaweza mleta mwandishi wa habari kwa jamii ili kuhakikisha kila mwana jamii anatumia haki yake vema",ameongeza Riziki.
Amefafanua kuwa katika mkutano huo wa siku mbili wadau watajadiliana kuhusu kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia na namna ambavyo umma unahusishwa kwenye uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa lakini pia watajadili changamoto zilizopo kwenye sekta ya habari na kuweka mkakati wa kuzitatua ikiwamo namna ya kuboresha maisha ya waandishi wa habari.
Riziki amesema Majadiliano hayo yana lengo la kuongeza ukaribu na ushirikiano baina ya waandishi wa habari na Jamii, pia kuibua hoja zitakazowaleta pamoja Jamii na waandishi wa habari katika kuwa na mpango kazi wa utekelezaji ili kuhakikisha kila mwanajamii anatumia vizuri nafasi ya uhuru wa kujieleza kupitia vyombo vya habari kwaajili ya maendeleo endelevu.
"MISA Tanzania inatarajia katika maboresho tunayofanya katika kutumikia umma na tasnia ya Habari ni pamoja na kuwa na mkutano kama huu kila mwaka na kuwa na jumbe tofauti tofauti kulingana na mada za mwaka husika, katika kuendeleza jitihada za Misa Tanzania kwenye ustawi wa tasnia ya habari Tanzania. Kauli mbiu mwaka huu ni: "Uhuru wa Kujieleza Msingi wa Haki Zote kwa Maendeleo Endelevu",amesema.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari- MAELEZO Gerson Msigwa akizunguza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Misa Tanzania leo Jijini Dodoma. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari- MAELEZO Gerson Msigwa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Misa Tanzania leo Jijini Dodoma.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari- MAELEZO Gerson Msigwa na viongozi mbalimbali wakiimba wimbo wa Happy Birthday Misa Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Misa Tanzania leo Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Misa Tanzania, Elizabeth Riziki akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Misa Tanzania leo Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Misa Tanzania, Salome Kitomari akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Misa Tanzania leo Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Bodi ya Uongozi ya MISA Kanda, Dk. Tabani Moyo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Misa Tanzania leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Bodi ya Uongozi ya MISA Kanda, Dk. Tabani Moyo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Misa Tanzania leo Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Internews,Agnes Kayuni akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Misa Tanzania leo Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Internews,Agnes Kayuni akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Misa Tanzania leo Jijini Dodoma.
Maadhimisho ya Miaka 30 ya Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara Tawi la Tanzania (MISA Tanzania) yakiendelea

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments