MAKAPUNI 40 YAKIGENI KUSHIRIKI MAONYESHO BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI MWANZA
Na Tonny Alphonce,Mwanza.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoa wa Mwanza Gabriel Mugini Chacha akizungumza na Waandishi wa habari hawapo pichani.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoa wa Mwanza Gabriel Mugini Chacha wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chemba hiyo ambapo wafanyabiashara 350 ni kutoka hapa nchini na wafanyabiashara 40 ni kutoka nje ya Tanzania.
Baadhi ya viongozi wa TCCI mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja.
Bw Chacha amesema katika maonyesho hayo yatakayofanyika katika uwanja wa Nyamagana Mkoani Mwanza kuanzia tarehe 26/08/2022 hadi 04/09/2022 wafanyabishara kutoka nchi za afrika mashariki za Kenya,Uganda na Burundi na nchi za China,India na Indonesia watashiriki maonyesho hayo
Karambi amesema sababu za maonyesho hayo kufanyikia katika uwanja wa Nyamagana kwa mwaka huu ni kuwapa fursa wananchi wa maeneo yote kushiriki bila tatizo lolote maonesho hayo kwa sababu uwanja huo upo katika ya jiji la Mwanza.
Huu ni mwaka 16 sasa TCCIA mkoa wa Mwanza wamekuwa wakiandaa maonyesho haya ya Biashara ya Afrika Mshariki na mwaka huu maonyesho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo lugha ya Kiswahili ni Nguzo ya Kukuza na kuendeleza Biashara,Viwanda na Kilimo Afrika.
No comments