WATOTO WANAOZALIWA NA VVU WAONGEZEKA BUCHOSA,SERIKALI YA WILAYA YAOMBA MUDA KUCHUNGUZA JAMBO HILO
Na Tonny Alphonce,Mwanza
Serikali ya
wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza imeomba kufatilia taarifa ya kuongezeka kwa
idadi ya Watoto wanaozaliwa na VVU iliyotolewa katika kikao cha baraza la
madiwani lililoketi wilayani humo ili
kujua sababu za kuongezeka kwa maambukizi hayo.
Katika
taarifa ya Kamati ya UKIMWI ya Baraza hilo ilionyesha watoto 86 wamekutwa na VVU huku Watoto 14
wakiendelea kupatiwa dawa ya kufubaza virusi vya UKIMWI.
Akichangia
ripoti hiyo diwani wa viti maalumu kata ya Nyahunge,Grace Erenest amesema
idadi hiyo ni kubwa na haikubaliki kwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa elimu kwa
kina mama wajawazito na wataalamu wa afya namna ya kuzuia maambukizi kutoa kwa
mama kwenda kwa mtoto.
Diwani wa viti maalumu kata ya Nyahunge,Grace Erenest akielezea mstuko wake baada ya kupokea taarifa ya idadi ya watoto wanazaliwa VVU kuongezeka.
'Taarifa
hii inashangaza sana inawezekana vipi mtoto azaliwa na maambukizi ya VVU wakati
idadi kubwa ya kina mama kwa sasa wanajifungua kupitia vituo vya afya,nahisi
kuna shida kwa wataalamu wetu wa afya’.alisema Grace.
Diwani
Grace amesema kwa namna Serikali ilivyowekeza katika sekta ya afya ni aibu
kusikia ongezeko la Watoto wanaozaliwa wakiwa na maambukizi ya VVU kwa kuwa
vifaa na mazingira mazuri ya mama mjamzito kujifungua salama yapo.
Akitoa
ufafanuzi juu ya taarifa hiyo DMO wa Buchosa Irene Mkerebe ameliomba baraza la
madiwani kumpa muda wa kufatilia suala hilo la kuongezeka kwa idadi ya Watoto
wanaozaliwa na VVU katika halmashauri ya Buchosa ili kupata ukweli kuhusu
taarifa hiyo.
DMO wa Buchosa Irene Mkerebe akitoa ufafanuzi kuhusu idadi ya watoto wanaozaliwa na VVU kuongezeka.
Irene
amesema anachojua ni kuwa idadi hiyo ya watoto 86 ni wale Watoto ambao
wamezaliwa na kina mama wenyewe VVU na wamekuwa wakipatiwa dawa ili kuwakinga Watoto
hao wasiweze kupata maambukizi kutoka kwa mama.
‘Ukiangalia
Watoto hawa huwa tunaendelea kuwapatia dawa katika kipindi chote hata wakati
ananyonya ili kuendelea kumkinga asije kupata maambukizi kwa maana hiyo niwatoe
hofu waheshimiwa madiwani ukiona mtoto anapatiwa dawa mara baada ya kuzaliwa
sio kwamba tayari kaambukizwa bali tunamkinga asipate maambukizi’.alisema
Irene.
Akizungumzia
vituo vya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU Irene amesema hadi sasa
kuna vituo 18 ambavyo vimekidhi vigezo vya kuwahudumia watu wanaoishi na VVU.
Tanzania
ina Watoto na watu wazima milioni 1.7 wanaoishi na VVU na mnamo 2019 kulikuwa
na maambukizi mapya ya VVU 77,000
nchini.
Kwa mujibu
wa utafiti wa kitaifa wa athari ya VVU wa mwaka 2018 idadi ya wanawake wote
waliohudhuria kliniki ya wajawazito saw
ana asilimia 98 .9 kati yao asilimia 92.4 walishauriwa juu ya hali yao ya
maambukizi ya VVU.
Makadirio
yanaonyesha kuwa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama na mtoto yamepungua hadi asilimia 8 mwaka 2015 na
kuongezeka hadi kufikia asilimia 11 mnamo mwaka 2020 kulingana na makadirio ya
UNAIDS dhidi ya malengo ya ulimwengu ya asilimia 5.
No comments