Breaking News

WANAHABARI MWANZA WATAKIWA KUTUMIA TAKWIMU KATIKA KUANDIKA HABARI ZA MAZINGIRA

Na Laurencia Bernard,Mwanza

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kuzuia na Kupiga vita Matumizi ya Dawa za kulevya na Uhalifu, (OJADACT) Edwin Soko amewataka Waandishi wa habari kutoa elimu kwa Jamii juu ya udhibiti wa mabadiliko ya tabia ya nchi na uhifadhi wa fukwe unaosababishwa na shughuli za binadamu,Ili kuzitendea haki kalamu zao.

Soko ameyasema hayo katika maadhimisho ya Siku ya takwimu  Duniani (Open Data Day 2022).Yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Open Knowledge Foundation kwa  lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya matumizi ya Data katika uandishi wao wa habari hasa zinazo husiana na fukwe.

'Tuna kila sababu ya kutoa elimu kwa jamii sisi wana habari kwa kuwa Fukwe zetu zilizopo katika ukanda huu wa Afrika Mashariki zinachangia uchumi kwa asilimia 57 hili si jambo dogo kama Fukwe zitachafuliwa ina maana mapato yatokananayo na Fukwe yatakufa',alisema Soko.

Soko amesema kukosekana kwa takwimu sahihi za madhara ya uharibifu wa mazingira ya Fukwe na mazingira ya kwa ujumla ni sababu moja wapo zinazo sababisha jamii kushindwa kuchukua tahadhari katika baadhi ya mambo likiwemo suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake Mratibu wa OJADACT TANZANIA Lucy Kilanga amesema matarajio ya taasisi ya OJADACT nikuona waandishi waanza kuibua habari zinazohusiana na Fukwe ziwa Victoria ambazo zimekuwa zikikumbwa na majanga mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa kina cha maji pamoja na uvamizi wa Magugu Maji.


'Tuna angalia sasa uwezekano wa kuwapata wafadhili ambao watatupa nguvu ili tuwawezeshe wanahabari muweze kuibua habari mbalimbali zinazohusiana na Fukwe mkitumia takwimu ili kuisaidia pia serikali na jamii mkuona ukubwa wa tatizo na namna ya kupambana na matatizo hayo'.alisema Lucy.

Maadhimisho hayo ya Open Data Day 2022 yamehudhuriwa na waandishi wa habari wapatao 30 kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya  mkoa wa Mwanza.

No comments