WADAU WA UVUVI BUSEKERA WAUPOKEA MRADI WA KUZUIA VIFO VYA WAVUVI KWA FURAHA
Na Tonny Alphonce,Busekera Mara
Wadau,Wamiliki
wa Mitumbwi na wavuvi wa Kijiji cha Busekela wilayani Bunda
mkoani Mara wameahidi kuchukua tahadhari za kiusalama wanapokuwa katika
shughuli zao za Uvuvi ili kupunguza
ajali za majini na vifo vinavyoweza kuzuilika.
Wametoa
kauli hiyo wakati wa utambulisho wa mradi wa kupunguza vifo vya wavuvi
vinavyotokana na kuzama maji katika Ziwa Victoria unaofadhiriwa na shirika Royal
National Lifeboat Institution (RNLI) kuroka wingereza na kutekelezwa na shirika
la usimamizi wa mazingira na maendeleo (EMEDO) uliofanyikia leo katika mwalo wa Busekera.
Akizungumza
wakati wa utambulisho wa mradi huo Diwani
wa kata ya Bakumi,Munubi Mussa amelipongeza shirika hilo la EMEDO kwa
kuwapelekea mradi huo ambao utawasaidia wavuvi waweze kufanya shughuli zao
katika hali ya usalama.
‘Kumekuwa
na matukio ya kuzama mara kwa mara na kupoteza wavuvi na mali kwa hiyo kwenye mradi
huu wananchi sasa wanapewa uelewa wa namna gani waweze kukabiliana na mazingira
yao’.alisema Diwani Mussa.
Zawadi
Song’ola ambae ni mmiliki wa Mitumbwi amesema wamekuwa wakichukua taadhari kabla
ya kuingia majini lakini kupitia mradi wa huu wa kuzuia ajali ya majini kuna
haja ya kuongeza vifaa vya uokozi katika mitumbwi.
Kwa upande wake meneja Mradi wa kutoka EMEDO Arthur Mugema amesema mradi huo utashirikiana na makundi mbalimbali yanayohusiana na uvuvi wakiwemo viongozi wa BMU kwa lengo la kuwa jengea uwezo wa kiongozi na kifedha ili waweze kutatua kero mbalimbali za wavuvi.
‘Mradi huu
ni wenu,sisi EMEDO ni wasimamizi tu kwa maaana hiyo tutawashirikisha katika
kila hatua na hata miaka 3 itakapopita
basi mradi huu uweze kuendelea bila tatizo lolote na hata wadau watakapohitajika
lazima kwanza tuanze na wenyeji’.alisema Mugema.
Nae mkurugenzi wa shirika la EMEDO Editrudith Lukanga amesema hatua ambazo wameanza kuzichukua wadau wa uvuvi katika Kijiji cha Busekela zitapewa nguvu na mradi huo ambao lengo lake ni kupunguza vifo vya wavuvi vinavyotokana na kuzama maji
Amesema pamoja
na mambo mengine lakini elimu itatolewa juu ya namna ya kujikinga na ajali za
majini ambapo wataalamu watatoa mafunzo ya kuogolea,namna ya kujiokoa na kuokoa
wengine ajali inapotokea pamoja na kutumia vifaa vya kujikinga kuzama.
Shirika la EMEDO hadi sasa limeutambulisha mradi wa huo katika ngazi ya Wilaya na sasa mradi umeanza
kutambulishwa katika ngazi ya jamii ambako ndiyo utekelezaji wake utafanyika
kwa kushirikisha jamii husika.
No comments