Tanesco Mkoa wa Mwanza yatoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya huduma mpya ya Nikonekt
Na Maridhia Ngemela MWANZA.
Shirika la umeme (Tanesco) Mkoani Mwanza limetoa elimu sahihi ya matumizi ya mfumo wa Nikonekt kwa wanachi ilikuwarahisishia upatikanaji wa huduma hiyo.
Afisa Mahusiano wa Tanesco Mkoa wa Mwanza Fraviana Moshi akitoa elimu kwa wananchi juu ya huduma ya NIKONECT
Afisa Mahusiano wa Tanesco Mkoa wa Mwanza Fraviana Moshi, alipokuwa akitoa elimu kwa wananchi leo hii Juni 8 amesema Nikonekt ni huduma ya maombi ya kuunganishiwa umeme kwa njia ya mtandao, inayomuwezesha mteja kupata mahitaji mbalimbali bila kufika katika ofisi za Tanesko.
"Mfumo huu unatumia njia tatu kufanya kazi katika USSD,Web portal na Mobile App,mteja anapaswa kuwa na kitambulisho cha NIDA ili aweze kupata huduma ya maombi ya umeme kupitia Nikonekt,hii itasaidia sana wananchi kuepukana na tatizo la kutapeliwa na vishika ambao wamekuwa wakichafua jina la Shirika hili,"alisema Fraviana.
Alisema faida za kutumia mfumo wa Nikonekt ni kumrahisishia mteja kupata huduma kwa urahisi inaokoa muda,inapunguza urasimu na mianya ya vishoka na ni rahisi kufuatilia ombi la mteja.
Akizungumzia upatikanaji wa umeme,Farda Mohammed ambaye ni mkazi wa Kirumba wilayani Ilemela mkoani Mwanza,amesema kumekuwepo na urasimu mkubwa katika kupata huduma ya kuunganishiwa umeme,kwakuwa mfumo wa Nikonekt umekuja katika muda sahihi kutokana na vishoka wengi kuwadanganya wateja wasiyokuwa na uelewa.
"Tulikuwa tunateseka sana kupata huduma ya kuunganishiwa umeme vishoka ndiyo walikuwa wamejaa na matapeli wanasumbua wananchi,tunaiomba Tanesco isimamie vizuri mfuomo huo,siyo ifanye vizuri mwamzoni alafu ukisha zoeleka inakuwa tena tabu kupata umeme,"alisema Farda.
Aidha Farda alisema Tanesco inapaswa kuwaangalia watu wa vijijini ambao katika kutumia masuala mazima ya mitando bado ni tatizo,hususani kama kujiunga na mfumo wa Nikonekt ambao bila jamii hiyo kupatiwa elimu ya kutumia digital wanaweza wakaendelea kubaki katika shida ya ukosaji wa umeme kwa kucheleweshewa.
Nao baadhi ya Wananchi wamelipongeza shirika la Tanesco kwa kuanzisha huduma hiyo ambayo itawarahisishia kupata umeme kwa wakati.
No comments