Breaking News

Waje watusaidie watoto wanauhitaji sana vitu mbalimbali.


Na Maridhia Ngemela, Mwanza

Mashirika na watu wenye uwezo wameombwa kujitokeza kutoa misaada kwa watu wasiyojiweza ili kuwasaidia wenye uhitaji.



Khadija Mjungi ambae ni mlezi wa kituo kinachokea watoto yatima cha Taufiq kilichopo Mkoani Mwanza Wilaya ya Ilemela amewaomba watu wenye uwezo na Mashirika mbalimbali kujitokeza kuwasaidia watoto hao ambao wanauhitaji wa vyakula,nguo ,maradhi wajitokeze kutembelea kituoni hapo ili kutoa sadaka zao.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea na uongozi wa msikiti wa Ibadhi uliowapelekea msaada wa vyakula kwa ajili ya kusherehekea siku ya Eid lifti.

Shekh wa msikiti wa Ibadhi Nouh Mousa amewasisutiza pia watu wawe na tabia ya kuwasaidia wenye uhitaji ikiwa ni njia moja wapo ya kuwafariji na kuwaondoshea upweke watoto hao.
 
Mousa amesema kuwa ni vema viongozi na watu wenye lengo la kutoa misaada wawatizame watoto yatima kwani wanapowatembekea na kuwapatia chochote wanafarijika na kuniona wapo katika jamii iliyo salama.

Viongozi hao wametoa misaada katika vituo viwili vya Taufiq na Markaz Ibun Masoud vilivyopo Wilaya ya Ilemela

No comments