SIKU 365 ZA RAIS SAMIA ZAIDI YA BILIONI 19 ZATUMIKA KUJENGA MADARASA 985 JIJINI MWANZA
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Siku 365 za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Mkoa wa Mwanza umepokea zaidi ya bilioni 20 kwaajili ya ujenzi wa madarasa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabliel akitoa taarifa ya miradi ya maendeleo ya mkoa wa Mwanza.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 6,2022 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabliel wakati wa kusoma taarifa ya miradi ya maendeleo Mkoani Mwanza kwenye maadhimisho ya mwaka mmoja wa Mh.Samia Suluhu.
Gabriel amesema kuwa madarasa hayo yamejengwa kwa kutumia fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa, kati ya fedha hizo sh. bilioni 19.7 ni kwaajili ya ujenzi wa madarasa 985 ya shule za sekondari.
Amesema madarasa yote yamejengwa kwa ukamilifu na yameisha anza kutumika kwani lengo kubwa ni kuboresha, kuimarisha elimu na kujenga Taifa la watu walioelimika.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria mkutano wa kuangalia Siku 365 za Rais Samia.
Akizungumza hali ya ulinzi na usalama Mhandisi Gabriel amesema Mkoa wa Mwanza kwa ujumla uko salama kwani matukio ya uhalifu,ulipizaji visasi,umiliki wa mali kwa nguvu na ukiukwaji wa sheria za Nchi yanaendelea kushughulikia kwa mujibu wa sheria,na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kwa amani na utulivu.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza Antony Dialo amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Machinga katika soko la mchafu kuoga lilipo Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza Maulidi Dalali,amesema ndani ya mwaka mmoja kundi hilo limetambuliwa na kurasimishwa sanjari na kujengwa mazingira mazuri ya kufanya biashara.
No comments