HABARI PICHA,WILAYA ZA ILEMELA NA NYAMAGANA ZAPATA WAWAKILISHI WA TAWFA.
Na Tonny Alphonce,Mwanza.
Wilaya za Ilemela na Nyamagana zimepata Wawakilishi wanne watakao wakilisha Umoja wa Kitaifa wa Wanawake Wavuvi (TAWFA) katika ngazi ya wilaya.
Wawakilishi wa TAWFA kutoka Wilaya za Ilemela na Nyamagana,kutoka kushoto ni Ela Lingstone Mwakilishi Msaidizi (W)
Wawakilishi hao waliochaguliwa ni Maimuna Rajabu na Ela Livingstone watakaowakilisha TAWFA Ilemela na Angelina Deogratius na Catherine Fransis ambao wataiwakilisha wilaya ya Nyamagana.
Picha ya pamoja ya Wanavikundi kutoka Ilemela na Nyamagana na viongozi wa Serikali pamoja na viongozi wa EMEDO.
Mkurugenzi Mtendaji wa EMEDO Editrudith Lukanga akiongea na washiriki wa mkutano wa kuwachagua Wawakilishi wa TAWFA.
No comments