EMEDO NA RNLI WAJA NA MRADI WA KUPUNGUZA AJALI ZA KUZAMA MAJINI KWA JAMII YA WAVUVI.
Na Tonny Alphonce,Mwanza.
Imeelezwa kuwa Jamii za Wavuvi laki moja wanaofanya
shughuli zao na kuishi pembezoni mwa
Ziwa Victoria ,Mia mbili Thelathini na Moja kati yao wanapoteza Maisha
kwa mwaka kwa kuzama majini.
Mkurugenzi Mtendaji wa EMEDO Editrudith Lukanga na Steve Wills Mkuu wa program RNLI wakitia Saini ya Mkataba wa miaka mitatu wa kutekeleza mradi wa kupunguza ajali za kuzama majini katika Ziwa Victoria
Idadi hiyo ya vifo huenda ikapungua kutokana na Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo Tanzania EMEDO na Taasisi kutoka Wingereza inayohusika na masuala ya usalama kwenye maji na uokoaji RNLI kuingia mkataba wa miaka mitatu wa kusaidia jamii za wavuvi.
Mratibu wa Mradi huo Arthur Mugema amesema EMEDO NA RNLI wamekubaliana kupitia mradi huo wa miaka mitatu waweze kufikia matokeo ya jumla hadi ifikapo 2025 na kuona wadau wakichukua hatua zinazofaa katika kupunguza matukio ya watu kuzama majini hasa kwa jamii inayoishi pembezoni mwa Ziwa Victoria.
Arthur amesema Mradi huu utatekelezwa katika vijiji 7 ambavyo vilichaguliwa kutokana na utafiti uliofanywa na kuvitaja vijiji hivyo kuwa ni visiwa vya Gozba na Mulumo vinavyopatikana Wilayani Muleba,Musozi na Irondo vinavyopatikana Ukerewe,Kome na Busekela katika Hlmashauri ya Wilaya ya Musoma na Sweya iliyopo Nyamagana Jijini Mwanza.
kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa EMEDO Editrudith Lukanga amesema mradi huu ni kwanza kufanyika Afrika ukiwa umelenga kutoa usalama kwa jamii za wavuvi wanaofanya kazi majini na waleo wanaoishi pembezoni mwa Ziwa Victoria.
Bi Lukanga amesema mradi huu pia unatekeleza sera mbalimbali zilizopo ambazo zinasisitiza suala la usalama wa wavuvi pamoja na suala la uvuvi endelevu.
Naye Steve Wills Mkuu wa program RNLI amesema mradi huu ni muhimu sana kwa sababu tafiti mbalimbali zinaonyesha watu wengi wanaofanya kazi za majini na wanaoishi pembezoni mwa maji wanapoteza maisha na kuziacha familia zikiwa hazijui nini cha kufanya.
Amesema kupitia mradi huu anaamini maisha ya jamii ya wavuvi itapatiwa elimu na hivyo itaweza kujilinda na kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vinavyotokana na kuzama majini.
No comments