20 WANOLEWA UANDISHI WA UCHOKONOZI UHALIFU WA MAZINGIRA
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
SERIKALI imesema kutokana na mazingira kuwa agenda ya kidunia imetoa kipaumbele kikubwa kwenye uhifadhi wa mazigira kwa kuandaa sera ya mazingira na kanuni kuhakikisha yanahifadhiwa na kuiwezesha jamii kuishi salama.Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Alfred Yonas,kwa niaba ya kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Hassan Masalla, akifungua mafunzo ya siku moja ya uandishi wa uchokonozi wa uhalifu wa Mazingira yaliyoandaliwa na Chama Cha Kupiga Vita Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) ikishirikiana na The Enviromental Reporting Collective (ERC) ya Malaysia, jijini Mwanza.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana,Yonas Alfred kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Hassan Masalla wakati akifungua mafunzo ya uchokonozi (IJ) wa uhalifu wa mazingira kwa waandishi wa habari 20 wa vyombo mbalimbali jijini Mwanza jana.
Alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,imetoa kipaumbele kwenye uhifadhi wa mazingira, inazo sera na kanuni mbalimbali zinazosistiza jamii kutunza na kuhifadhi mazingira yawe salama na endelevu.
Hivyo, Chama Cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kuandaa mafunzo hayo ya uchokonozi kikishirikiana na Shirika la Kimataifa la The Enviromental Reporting Collective (ERC) la Malaysia,kimeona mbali kuwa yana maslahi kwa taifa letu kuhusu mazingira.
Alfred alisema uhifadhi wa mazingira ni agenda ya kidunia kwa sasa na bila kuyatunza ni wazi viumbe hai akiwemo binadamu kesho haiwezi kukamilika,hivyo uandishi wa habari za uchunguzi wa uhalifu kwenye mazingira ni muhimu na utasaidia kuibua uhalifu wa mazingira.
“Mfano Wilaya yetu ya Nyamagana na Mkoa wa Mwanza una changamoto nyingi za uhalifu wa mazingira,uvuvi haramu kwenye Ziwa Victoria,ukataji miti ovyo ili kupata nishati ya mkaa,uchafuzi wa anga ya ozon na matumizi ya kemikali migodini,baada ya mafunzo nendeni mkatumie kalamu na elimu mtakayopata mkafichue uhalifu huo,”alisema Alfred.
Katibu Tawala huyo alisema washiriki wa mafunzo hayo watabobea kwa kuandika habari za kuibua uhalifu wa mazingira,sababu mahitaji na changamoto zinaongezeka na kubadilika,hivyo habari ziwe zenye tija na kuibua mengi yanayoweza kufanyiwa utafiti kwenye vyuo vikuu ili kuleta mabadiliko katika jamii na taifa letu.
“Mtasaidia kuielimisha jamii kuelewa umuhimu wa kutunza na kulinda rasilimali, misitu, wanyama na mazingira na kuyafanya endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo,zamani jamii iliishi karibu na mazingira nayo yakaitunza hivyo mkifanya hayo mtakuwa mmeisaidia sana jamii na serikali kuleta maendeleo,”alisema.
Alitoa rai kwa waandishi kuwa wabunifu a kuendelea kupata na kutoa elimu ya mazingira kwa maslahi ya nchi ikizingatiwa taaluma hiyo ni chanzo na masikio ya serikali, pia shule ya jamii katika kuchochea na kuchagiza maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake Mwezeshaji, Lucyphine Kilanga, alisema baada ya miaka 20 ijayo Tanzania tunaweza kupata madhara makubwa ya hewa ya Oxygen kutokana kuharibiwa kwa anga hewa ya Ozon na kukata miti ovyo,ili kulinda mazingira yaendelee kuwa salama jamii iepuke kukata miti ovyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Kupiga Vita Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) Edwin Soko,akitoa neno kwa waandishi wa habari washiriki wa mafunzo hayo (hawapo pichani) yaliyoandaliwa na chama hicho kwa kushirikiana na The Enviromental Reporting Collect ive (ERC) ya Malaysia, jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa UNEP, zaidi ya tani 300 milioni ya uchafu unaotokana na plastiki zinazalishwa duniani kila mwaka kwa sababu plastiki haziozi kwa haraka, hivyo hazipotei zinapotua ardhini au majini, hubaki na kuendela kuwa ndogo ambapo tafiti zimeonyesha kuwepo kwa plastiki ndogondogo katika Ziwa Victoria na kwenye samaki baadhi huishi nazo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya habari za uchonokozi wa uhalifu wa mazingira jijini Mwanza jana,mafunzo yaliyoandaliwa na Chama Cha Kupiga Vita Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kikishirikiana na The Enviromental Reporting Collect ive (ERC) ya nchini Malaysia.
Hata hivyo,habari za uchafuzi unaotokana na plastiki ndogo ndogo katika nchi za Maziwa Makuu Afrika, haziandikwi kwa wingi ukilinganisha na nchi nyingine duniani na hapa nchini zimeanzishwa kampeini za mazingira katika mikoa mbalimbali,zikilenga kuhamasisha watu kuendelea kuhifadhi na kulinda maeneo yao bila uharibifu wa mazingira.ssssss
No comments