Breaking News

PICHA,KONGA YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA YAPONGEZWA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI

Tonny Alphonce,Musoma..

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Msuala ya Ukimwi,Madawa ya Kulevya na Kifua kikuu Bi Fatuma Hassan amekipongeza kikundi cha watu wanaoishi na VVU cha Halmashauri ya Manispaa ya Musoma kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutoa elimu kwa jamii juu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU.

Bi Fatuma amewataka wana Konga wa Mnispaa ya Musoma kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili iache kuwarubuni watoto wadogo na kufanyanao mapenzi kwa kuwa kwa kufanya hivyo kunachangia maambukizi mapya kutokana na kundi lingine ambalo nalo huwafata watoto hao wadogo na kufanyanao ngono zembe  wakidhani wapo salama kumbe nao tayari wameambukizwa.


Amewataka pia wana Konga kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kupima na kutumia dawa kwa usahihi kwa kwa kuwa kupata maambukizi sio mwisho wa maisha.

Mkurugenzi Mtendaji wa NACOPHA,Bw Deogratius Rutatwa akijitambulisha mbele ya wajumbe wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Msuala ya Ukimwi,Madawa ya Kulevya na Kifua kikuu Bi Fatuma Hassan akizungumza mara baada ya kujionea vitu vinavyozalishwa na watu wanaoishi na VVU.

Wana Konga ya Musoma wakifurahia jambo.



Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI wakijitambulisha.










No comments