MKURUGENZI MTENDAJI WA NACOPHA ATAKA KUONGEZWA BAJETI YA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI
Na Tonny Alphonce,Mara
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Bw Deogratius Rutatwa ameitaka Kamati ya Bunge ya masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya kuongeza bajeti ya kupambana na ugonjwa wa UKIMWI.
Amesema Kwa Mkoa wa Mara kiasi kilichotengwa upande wa mwitikio wa UKIMWI ni asilimia 7 tu kiasi ambacho ni kidogo sana.
Bw Rutatwa amewaomba wabunge wa kamati ya UKIMWI kuishawishi serikali itenge fedha za kutosha Ili Taifa liweze kufika malengo ya sifuri tatu.
Amewataka pia viongozi wa kisiasa na wataalamu kuwa makini kwenye matamshi yao kwa kuwa matamshi mengine yana wanyanyapaa Watu wanaoishi na VVU.
"Unaposema kupatikana Kwa Virusi ya UKIMWI ni shida au tatizo hii itasababisha Watu kuacha kupima na hapo tutazidi kuongeza tatizo"alisema Bw Rutatwa.
kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya masuala ya UKIMWI Bi Fatuma Hassan amesema changamoto walizonazo watu wanaoishi na VVU mkoani Mara wamezisikia na kuutaka uongozi wa mkoa uangalia namna ya kutatua baadhi ya changamoto zinazowekana ikiwemo ya kupata mashine ya kupima uwingi wa virusi mwilini.
No comments