Breaking News

Jumuiya ya vijana wa kiislam Mkoa wa Mwanza wajiandaa kupokea mwezi mtukufu wa Ramadhan.



Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Jumuiya ya vijana wa kiislam mkoa wa Mwanza wamefanya mazoezi ya viungo leo hii 27 katika uwanja wa michezo Nyamagana kwa lengo la kujiandaa kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhan unaotarajia kuanza hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana Mkoa wa Mwanza Bakarani Omary alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mazoezi hayo amesema kuwa lengo la kuanzisha mazoezi hayo ni kuwajengea uwezo na tabia ya  kuwa wanafanya mazoezi ili kuwa na afya imara Kuelekea mwezi wa Ramadhan na zoezi hilo litakuwa endelevu.

Amesema kuwa, wameamua kuliganya jambo hilo ilikuwa na utamaduni wa kuwana muendelezo wa kufanya mazoezi na kuwa na afya imara na ameishukru Banki ya Crdb kwa kuwadhamini na kuwafungulia akaunti ya Albaraka ambayo haina riba iliyofuata utaratibu wa dini ya kiislam.

Nae Meneja wa  tawi la banki ya CRDB Mwanza Jeremiah Msemwa amesema kuwa wameamua kufungua dirisha la Albaraka yenye lengo la kuwahudumia wananchi wote wakiwemo waislam kutokana na dini hiyo kutokuwa na Sheria ya  kutoza riba kwani ni haramu.

Msemwa amesema kuwa dirisha hilo halibagui linahudumia dini zote kwa wale wasiyopenda riba kutokana na imani zao za dini  hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujivunia huduma hiyo ambayo inauwezo wa kupata huduma za mikopo ambazo zinafuata misingi za dini ya kiislam.

Rajabu Hahaha ni Mwenyekiti wa Efm joging amesema kuwa lengo la niwashawishi watu kufanya mazoezi nikuwajengea uimara wa afya bora na kuwaelimisha kuweka akiba zao.

No comments