Breaking News

Wananchi wametakiwa kutambua alama zinazobandikwa kwenye bidhaa.

Na Hellen Mtereko, Mwanza


Wananchi wametakiwa kutambua  alama maalum inayobandikwa katika bidhaa ili kuonesha uhalali wa bidhaa wanazotumia kwa lengo la kutunza afya zao. 



Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari.


Rai hiyo imetolewa na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Alphayo  Kidata alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Leo hii Febuari 14,2022 Jijini Mwanza.


Amesema bidhaa zinazoingizwa hapa Nchini na wafanya biashara wanaotambulika lazima ziwe na alama maalum za stempu za kielectroniki.


Kidata ameongeza kuwa,wananchi wanaotumia bidhaa hizo  washirikiane kwakulinda afya zao kwa kutambua bidhaa halisi na halali kwa matumizi kwa kutumia simu zao za kiganjani kabla ya kutumia bidhaa hizo.


Amefafanua kuwa,faida moja wapo ya ETS ni kulinda afya ya mtumiaji kwa kujiridhisha kuwa bidhaa hiyo imezalishwa na nani,lini na itakuwa imepita katika  vyombo vya udhibiti wa ubora wa Serikali na kuhakikisha Kodi ya Serikali inalipwa kupitia kwa wazalishaji wanaotambulika na sii udanganyifu.


Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imewaomba wananchi kupakua App ya hakiki stempu kwenye simu zao za kiganjani Bure ambayo itawawezesha kutambua bidhaa  isiyofaa na kuiwezesha Serikali kukusanya mapato yatakayo saidia kujenga miradi mbalimbali hapa Nchini.



No comments